Salama.
Kiukweli nawaonea huruma CCM chama cha siasa kwa namna wanavyohangaika huku na huko kutafuta mapenzi kwa wapiga kura kwa gharama kubwa sana na wananchi kuwashawishi pasipo maana.
CCM jichunguzeni kupitia mifano na kazi zilizopita. Fanyeni mchanganuo sahihi na bora kuhusu wananchi kwa ujumla wanawazungumziaje matendo yenu na siasa mnayoitumia kuhudumia na kutatua changamoto zao.
Changamoto kubwa inayowasumbua CCM kwasasa na haiwezi kukwepeka ni ongezeko kubwa la wasomi nchini linalopelekea siasa zenu za ahadi uongo, sera za kufirika, tambo, umaarufu na mambo yanayoendana na hayo kuwa kikwazo kwa CCM kujitetea kwa wananchi na wapiga kura halisi.
1. Nchi hii ilikuwa na viwanda lukuki karibia kila mkoa na mazao ya kimkakati, CCM kwa uzembe wenu mkaua kila kitu.
2. Nchi hii wasomi mbalimbali walipata ajira ya moja kwa moja kutoka vyuo walivyosoma kwenda idara na taasisi mbalimbali nchini, CCM mkavuruga utaratibu wote na kuwaweka watoto wenu, ndugu na jamaa zenu mkaharibu kila kitu na kusababisha tatizo la ajira nchini.
3. Nchi hii ilikuwa na vyuo vya kuandaa viongozi na watawala, CCM mkavurugavuruga kila kitu na kuanza kuchaguana chaguana kwa uchama na uswahiba.
4. Nchi hii sera ya biashara na uwekezaji wakati huo ilikuwa rafiki, CCM mkaanza kukwepa kodi na kufungua biashara zisizo halali yaani walio wengi wenu wenye mamlaka mkavuruga vuruga ovyo ovyo ndio chanzo cha ninyi CCM kuwa na mrundikano wa kodi na ushuru usio maana.
NB
CCM brothers & sisters, it's too late to apologize royal voters.
Tanzania nchi tamu sana.