Ushauri: CHADEMA andaeni maandamano kupinga Kikokotoo tu kwa idara zote na mtaungwa mkono

Ushauri: CHADEMA andaeni maandamano kupinga Kikokotoo tu kwa idara zote na mtaungwa mkono

Waguswa kikotoo wengi ni watumishi wa umma. Wao wamejaa uoga na unafiki, hawataweza kuandamana. Waandamanaji ni wenzangu na mimi, watajiuliza kinatuhusu nini kikokotoo.

Waandamane kuhusu gharama za maisha, kikokotoo iwe ajenda ya kuzungumzwa tu lakini sio main subject matter
 
Kote barani wanatucheka kwa kuendelea kutawaliwa na ccm huku wananchi tukiwa hoi. Magufuri alijitoa ifahamu ndiyo barabara aliweza kijenga. Kwanini hatufahamu Hilo.
 
Mleta mada ana hoja ya msingi lakini sikubaliani na yeye kuwabebesha huo mzigo CHADEMA. Wakati CHADEMA wanapigwa na kufunguliwa kesi kwa kuwatetea wanyonge wakiwamo waathirika wa kikokotoo wafanyakazi wa nchi hii wao wapo kimya wanakula kiyoyozi ofisini. Na mbaya zaidi baadhi ya waathirika wa hicho kikokotoo ni walimu na polisi ambao ndio wanaoongoza kuwaumiza CHADEMA na vyama vya upinzani kwa ujumla wakiwa wao ndio wasimamizi wakuu wa moja kwa moja wa uchaguzi.

Kwa hiyo mleta mada wewe na waathirika wenzako watarajiwa wa kikokotoo bado hamjachelewa sana bali fanyeni yafuatayo:-
1. Andaeni mabango/bango yenu tafuteni wawakilishi wakayabebe Mwanza, Mbeya na Arusha ujumbe utafika.
2.Kwenye vyama vyenu vya wafanyakazi chagueni viongozi ambao wataibeba ajenda na maslahi yenu badala ya kuchagua machawa ambao huishia kusifia tu.
3. Kama viongozi wenu hawawatetei undeni kamati yenu ya dharura nje ya uongozi ili ikafanye mazungumzo na viongozi wa juu serikalini bila kukata tamaa kwani ipo siku viongozi wa nchi hii watasikia malalamiko yenu na ya kuyafanyia kazi. Hoja hii najua watu wengi wataipinga lakini naamini kati ya viongozi waliopo bado viongozi waadilifu wapo na muasisi wa taifa hili alitufundisha kupambana kwa hoja mpaka kieleweke.
4. Mleta mada na wenzako nendeni kwenye mikutano ya mwenezi huenda suala lenu likapatiwa ufumbuzi kwani ameshatatua matatizo mengi na mengine makubwa kuliko hili la kwenu la kikokotoo. Nafikiri hili likifika kwake chama kitaiuliza serikali kwa nini inaumiza wastaafu wa nchi hii ambao wametumikia nchi kwa muda mrefu tena kwa uadilifu mkubwa.

Ni mtizamo tu
 
CHADEMA kama kweli maandamano yenu ni ya dhati toka mioyoni basi maandamano yatakayofuata kuanzia maandamano yajayo fanyeni maandamano makubwa, kushirikisha taasisi zote za serikali ambazo zimeathiriwa na kikokotoo japo taasisi hizo haziwezi kushiriki moja kwa moja ila zitawaunga mkono kwa namna yeyote ile.

Manake CCM wanategemea hizo taasisi katika kusimamia uchaguzi, na kuwalindia kura katika chaguzi zote, hasa Polisi, walimu ndio wanatumika sana na hao ndiyo waathirika wa kikokotoo.

Kwahyo inatakiwa mshinikize hizo taasisi ziungane na ninyi hata kwa fikra, vitendo na pia fanyeni iwe ajenda yenu kuu kwa sasa.

Niwaambieni kwakua leo taasisi zote zimesema mtu, au chama kitakachoenda na Agenda ya kikokotoo ndicho wataenda nacho au wataenda nae.

Agenda ya kikokotoo ni muhimu kuelekea uchaguzi, na Agenda ambayo wabunge wa ccm wameshindwa itetea, wangeitetea ingekuwa kura muhimu kurudi bungeni.

Sikupaswa kuweka hili suala hadharani kwakua nimeweka silaha hadharani na adui kaona CCM,kwakua CCM ni bingwa wa kutengeneza tatizo na kutatua mwakani wataibeba kama Agenda muhimu ili wachaguliwe.

Na ushauri wangu wa mwisho mkihachana na maandamano anzeni kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano, itisheni makongamano kama ya katiba mfanyavyo ila yawe kwajili ya kutoa elimu kuhusu kikokotoo, mathara yake kwa wafanyakazi hakika itakuwa ni kete muhimu kwenu na mtarudi kwenye mstari.

KHERI YA MAANDAMANO KWA SIKU YA LEO
MWENYE:MATULANYA MPUTA
Email:maggierozaria@gmail.com
si na wewe uanzishe? why chadema chaema?
 
Mleta mada akili huna kikokotoo kinahusu hao wafanyakazi wengi wa Umma ambao hawafiki laki nne jumla kwenye Nchi yenye watu milioni 60 .Wapuuzi hao hawajali wananchi Wana nyodo maofisini wananchi wakienda Kutaka huduma wanajiona miungu watu kuanzia traffic barabarani,TRA,Halmashauri ,Maafisa Ardhi , Hospital nk hakuna mwananchi atawaunga mkono zaidi ya kuwapopoa Mawe na matusi ya nguoni wakiandamana sababu hawana faida yeyote kwenye utatuzi wa kero za wananchi

Ziara ya Makonda ukiona wananchi wanavyowaona kero hao watumishi wa Umma wakiandamana Kwa kikokotoo Chao wajiandae kuzomewa na kupopolewa na Mawe na wananchi wenye hasira wasio hudumiwa nao vizuri
 
Tatizo ni kwamba nyie Watoa ushauri wala hamtashiriki because mtakua maofisini
hata wasiposhirikie mandamano ,wabunge na madiwani watakaogombea nakuhakikishia wakija na ajenda hii MUHIMU ,CCM iaweza kung'oka maradakani au upizani kupata kura nyingi sana.hakuna ajenda MUHIMU kama hii. ajenda ya kugawa nji kwa majimbo huwa haina mashiko kabisa.njoni na ajenda hii muhimu .
 
Mleta mada akili huna kikokotoo kinahusu hao wafanyakazi wengi wa Umma ambao hawafiki laki nne jumla kwenye Nchi yenye watu milioni 60 .Wapuuzi hao hawajali wananchi Wana nyodo maofisini wananchi wakienda Kutaka huduma wanajiona miungu watu kuanzia traffic barabarani,TRA,Halmashauri ,Maafisa Ardhi , Hospital nk hakuna mwananchi atawaunga mkono zaidi ya kuwapopoa Mawe na matusi ya nguoni wakiandamana sababu hawana faida yeyote kwenye utatuzi wa kero za wananchi

Ziara ya Makonda ukiona wananchi wanavyowaona kero hao watumishi wa Umma wakiandamana Kwa kikokotoo Chao wajiandae kuzomewa na kupopolewa na Mawe na wananchi wenye hasira wasio hudumiwa nao vizuri
hahahahha.akili anazo .hataka kama zingekuwa kidogo usimtusi.mfano wa swali natamani kujua ni kwamba ,mstaafu akifa kabla ya ile miaka 12 yakuendelea kupewa pensheni zile hla zinazobaki anapewaga nani?
halafu swala hili siyo tu watumishi wa umma bali hata watumishi wa secta binafsi .

unajua kikokotoo kingesema anagalau ukistafu unapewa 50% ya hela zote hapo sawa .maana kwa mfano mtumi kwenye secta ya binafsi huwa anakatwa 10% mshahara wake kwenda hifadhi ya jamii( NSSF au PSSF ) na mwajiri anamchangia 10%.sekalini ni tofauti . mtumishi anakatwa 5% na serikali inamchangia 15%. sasa ukistafu eti wakupe 33 % ? sijajua ni sababu gani BUnge liliona ni sahihi mtumishi huyu apewe 33% .ni afadhali apewe 50% ,inayobaki hata akipewa kidogo sioni shida.kusema kweli mimi huwa natamani kuacha kazi nifanye mambo yangu mapewa kuliko kukaa 60years then hela zangu nilizovujia jasho unipe 33% eti nyengine utanipa kidogo kidogo.
 
Haiwezekani waka-address hoja na matamanio yako yoootee kwa siku moja.Ngazi kwa ngazi.Halafu,hata wewe unaweza kuitisha maandamano utoe/uweke hoja zako.Usiwatwishe CHADEMA kila kitu.Chukua nafasi yako.
Akili zako ndogo, mtu uitishe maandamano umesajiliwa Kama chama cha siasa? Chama cha wafanyakazi?
Utaitisha kwa utaratibu gani?
 
Akili zako ndogo, mtu uitishe maandamano umesajiliwa Kama chama cha siasa? Chama cha wafanyakazi?
Utaitisha kwa utaratibu gani?
Ataomba miongozo na kupewa.Wewe ndiye unafikiria kwa kudeka hadi kujipa majina kama mpunga mashetani.Ukiambiwa kitu kimoja unapaswa kufikiria vitu sita zaidi.Acha ukarunguyeye wewe vipi?Yeye kabisha na kuogopa?Sutpid mwili mzima.
 
hahahahha.akili anazo .hataka kama zingekuwa kidogo usimtusi.mfano wa swali natamani kujua ni kwamba ,mstaafu akifa kabla ya ile miaka 12 yakuendelea kupewa pensheni zile hla zinazobaki anapewaga nani?
Na wewe aikili huna aliyekwambia pension mwisho miaka 12 nani? Ujinga wako peleka huko.Pension mtu analipwa Hadi akifariki sio miaka 12 ni afya yake tu aweza hata Aishi miaka 50 baada ya kustaafu ataendelea kulipwa tu

Na wengi pension ambao afya zao ziko vizuri pension walizolipwa zinapitiliza michango Yao yote waliyochangia wakati wakiwa kazini.Mfano mtu alifanya kazi miaka 10 akastaafu akiwa na miaka 60 akaishi miaka 100 pension ya Kila mwezi aliyopewa miaka hiyo 40 inazidi michango yake alichangia mara zaidi ya 800.kuwa wangehesabu tu michango yake pension yake ingekata baada ya miaka sita tu chake chote alichochangia miaka yote kingeishia hapo

Pension haikatiki Hadi ufe
 
hata wasiposhirikie mandamano ,wabunge na madiwani watakaogombea nakuhakikishia wakija na ajenda hii MUHIMU ,CCM iaweza kung'oka maradakani au upizani kupata kura nyingi sana.hakuna ajenda MUHIMU kama hii. ajenda ya kugawa nji kwa majimbo huwa haina mashiko kabisa.njoni na ajenda hii muhimu .
Wanailetaje kWa mfano wakati waajiriwa nchi hii wanaofikia Umri huo hawafiki hata 10% ya voters?

Wangapi wana ajira rasmi Tanzania ?

Hiyo agenda haiangushi mbuyu
 
Back
Top Bottom