Ushauri: CHADEMA mwaka 2025 nendeni na Freeman Mbowe nafasi ya Urais

Ushauri: CHADEMA mwaka 2025 nendeni na Freeman Mbowe nafasi ya Urais

SHILLINGS

Senior Member
Joined
Oct 24, 2013
Posts
160
Reaction score
648
Baada ya kufikiria mwenendo wa vyama vya upinzani Tanzania hususani CHADEMA pasipo shaka nimejiridhisha kwamba Mhe. Freeman Mbowe ndio anafaa kupeperusha bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo hasa baada ya kifo cha Hayati Joseph Pombe Magufuli. Mbowe ameonyesha kukomaa kifikra hasa katika kipindi hiki cha maombelezo ya msiba. Ameonyesha ni mwanasiasa iyeiva, mwenye busara ya hali ya juu tayari kwa majukumu mazito ya kuliongoza taifa.

Pamoja na ukomavu huu, haiba na historia yake ya kiasiasa ikiwa ni pamoja na misimamo yake ya kutoyumbushwa kwa fedha ni moja ya ishara kwamba ni mwanasiasa anayeamini katika kile anachokipigania. Bila shaka kama sio Freeman Mbowe kusimama imara CHADEMA kingefutika kabisa. Halima Mdee na wenzake wamethihirisha pasipo shaka kwamba nguvu ya fedha ni kipaumbele kuliko uimara au heshima ya chama. Freeman Mbowe ni mbegu halisi ya CHADEMA na kiongozi mwenye stamina za kuhimili mikikimikiki ya siasa kwenye nchi hii.

TAHADHARI:

- Kwanza, Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo ni binafsi sana kwa Mbowe ambavyo anaweza kuvirekebisha hususani kwa kuchuja kwa uangalifu watu wanamzunguka. Vitu hivi wapinzani wake wakisiasa huvitumia kumjengea propaganda. Tuliona alivyoweza kuyumbishwa kwa propaganda siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambazo zilijenga taswira hasi dhidi yake.

- Pili, propaganda ya ukabila inatumika sana hususani kwa wachaga, ambayo imefanyika kwenye tawala zote na ilishika kasi zaidi kwenye awamu ya 2015 - 2020. Mbowe anapaswa kutambua hili kwake ni kikwazo ambacho anapaswa kukifanyia kazi.

USHAURI kwa CHADEMA, anzeni kuandaa wagombea wenu mapema hususani kwa upande wa Urais wakati mkiendelea na mapambano mengine ya kudai katiba, tume huru ya uchaguzi n.k. Anzeni kuonyesha kwa vitendo fikra mbadala kwa kuwa na agenda nzuri kwa makundi mbalimbali ya kijamii hususani tabaka la chini kabisa la wakulima na wafugaji.

Nafasi ya Urais inahitaji mtu/watu walioandaliwa kwa kipindi cha kutosha na kujengwa kisiasa "political branding" ili kuuzika kirahisi kwa wananchi. Ninapoitazama CCM ya sasa na ninapomtazama Freeman Mbowe naona kabisa ana nguvu ya kutosha kukabiliana na mgombea yoyote wa Chama hiki kikongwe cha siasa Tanzania na Afrika.
 
Back
Top Bottom