Sio kwa nia mbaya au kuwapangia mambo; CHAUMMA kwa hadhi yenu nyie sio wa kushindwa kutengeneza website hata ya bei kidogo ili kuenda na wakati wa sasa wa Teknolojia ya mawasiliano na kuleta udhibiti wa mawasiliano yenu ndani ya chama chenu.
Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Kurugenzi ya Uenezi na Mawasiliano ya chama kutumia "Gmail" hakuendani na hadhi ya chama chenu na hadhi ya watu waliopo ofisini.
Haiba ya chama chochote makini kwa ulimwengu wa sasa wa kidigitali, ni publicity/uenezi na namna kinavyodhibiti mawasiliano yake ya ndani na nje.
Kuleni ubwabwa ila msisahau hili la website. 😊
View attachment 3593049
Mkuu, umeeleza tu faida za kuwa na website; ungetaja pia hasara zake ingependeza zaidi ili wenyewe waamue kwa busara kuwa na website au kuendelea kutumia gmail.
Actually, website yenye domain ya .co.tz ni “public presence tool”, sio lazima iwe mbadala wa mfumo wa mawasiliano; Gmail ni communication tool, wakati website ni information platform. Hivyo nafikiri kuzi-compare moja kwa moja ni kuchanganya majukumu tofauti.
Disadvantages za kuwa na website vs kutumia gmail: Website inahitaji maintenance ya mara kwa mara (hosting, updates, security patches, uptime monitoring), wakati Gmail ni managed system ambayo haimhitaji mtumiaji kuhusika na technical upkeep yoyote.
Gharama za website ni endelevu: domain, hosting, na mara nyingine developer au admin wa IT; Gmail kwa upande mwingine ni zero-cost kwa matumizi ya msingi na ina infrastructure tayari.
Website inaweza kushuka (downtime) kutokana na server issues, traffic overload, au configuration errors; Gmail ina kiwango cha juu sana cha reliability kwa sababu iko kwenye global infrastructure ya Google.
Website ni nzuri kwa “broadcasting information” (taarifa kwa umma), lakini sio efficient kwa mawasiliano ya haraka, direct, na two-way interaction kama Gmail inavyofanya.
Usimamizi wa website unahitaji technical skills (DNS, hosting control panels, CMS updates), wakati Gmail inaweza kutumiwa na mtu yeyote bila maarifa ya IT.
Website inaongeza visibility ya taasisi, lakini haiongezi automatically ufanisi wa kazi za kila siku; ni zaidi ya “presentation layer” kuliko operational tool.
By the way, mtu anaweza kula ubwabwa kila siku, lakini akakosa hela ya kutengeneza/ku-maintain website. Labda pia hao wanajali zaidi uhai wa tumbo kuliko hadhi. If so, yamkini budget yao inaelekezwa zaidi kwenye ubwabwa kuliko kujenga/kulinda hadhi.
Hapo vipi, mkuu.