ushauri... DISCONTINUE KWA MWANAFUNZI WA MWAKA WA NNE?

samuel faraj

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
1,326
Reaction score
1,265
Jaman husika na kichwa cha habari hapoa juu mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa nne UDSM(COET) kuna mwanafunzi mwenzetu wamemdisco chuo eti kisa cmu , alikutwa na simu kipindi cha ue na simu yenyewe aliingia nayo bila kujua ,simu ilikua ON kabisa haina uwezo wowote wa ku browse material kwenye net, sasa cha ajabu senate ya chuo wamekaaa ijumaa tar 5th april 2013 wameamua kum disco, tumebakiza miezi miwili tu kumaliza chuo je hii ni halali kweli?? Maamuzi waliyofanya ni sahihi wana JF tunaomba mawazo yenu tuweze kumsaidia mwenzetu kwani amechanganyikiwa hauju cha kufanya.Ushauri wenu plz
 
Kama simu ipo kwenye regulations za mitihani kwamba inazuiwa kuwepo kwenye chumba cha mtihani NI HALALI KABISA ADISCO, kWANI KAMA ENGINNEER inaonesha kwa kiasi ganin hayuko makini HAWA NDIO CHANZO CHA KUTUUA KWA KUJENGA MAJENGO CHINI YA VIWANGO kwa mfano tu. Hapa suala la Umakini limekoseakana mkuuu, akose Upolisi ambayo hapa kwetu imeonekana ndio kazi iliyokosa umakini na kazi ya makosa
 
Nope sio umakini mkuu as you know sisi binadamu we are nt perfect makosa ya kibinadamu kama hayo yapo even machine hazipo perfect thus why efficiency yake is not 100%
 
Ndio upumbavu wa vyuo vya kibongo yaaani mtu kasoma miaka 4 yote halafu wanamdisco bora wamwambe arudie mwaka
 
Mpe pole, kanuni nyingi za mitihani haziruhusu mtu kuingia na simu. You can not browse internet, but you can send and receive sms from your colleagues.
 
Tatizo kubwa ni namna gani msimamizi angeweza ku-prove kwamba mwanafunzi alienda na simu kwa bahati mbaya hakuwa na nia ya ku-cheat!! Kuna vitu vingi ambavyo Senate inaweza kuwa imeviangalia kabla ya kufikia uamzi wa kum-discontinue. Pengine pia kunaweza kuwa na details zingine ambazo hazijawekwa wazi ambazo zilichangai kum-discontinue. Ushauri wangu: kama mwanafunzi hakuridhika na decision ya Senate, nadhani, kama sheria hazijabadirika, anaruhusiwa ku-appeal against the decision made. I sympathize with him. Kama alivyosema mchangiaji mmoja, umakini unakosekana kwa vijana wengi siku hizi.
 
Wanamdisco mwanafunzi wa masters mbaba mwenye mke na watoto. Tena tutorial assistant wa chuo kingine. Walimu wa chuo akili zao ni nywele tu. Ukiona ana kipara stuka.
 
Ndio upumbavu wa vyuo vya kibongo yaaani mtu kasoma miaka 4 yote halafu wanamdisco bora wamwambe arudie mwaka
Nyakipambo, unaweza kutoa mifano ya vyuo viwili tu vya nje ya bongo ambavyo vinakubaliana na ukiukwaji wa examination regulations halafu wanamruhusu mwanafunzi husika arudie mwaka? Ninachofahamu mimi ni kuwa mwanafunzi anaweza kupewa hata award lakini ya chini tofauti na ile aliyokuwa anaitafuta pale ambapo anaonekana kafail kwa kukosa uwezo wa kupata kile alichokuwa anakitafuta lakini siyo kwa ku-violate exam. regulations, tena wenzetu ni wakali tofauti na unavyofikilia. Ukikamatwa tu, the next flight back home is yours!!
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na ww kaka bt inabidi waangalie circumstances iliyofanya mpaka huyo mtu akaingia na cmu kweye chumba cha mtihani je ilikua planned or ilitokea bahati mbaya, coz tunajua hata makosa ya mauaji yote yanakuwa ya mauaji bt kuna kukusudua na kutokukusudia,
 
i raealy smpathyz with him..!
Kuna movie moja ya kihindi inaitwa 'three ------' ndio nairelate na hili tukio!..unaweza kujicommit suecide hivhiv ila naomba asifikie huku
Actualy kukamatwa na cm ni kosa na hata kabla hamjaanza mtihani you are regular reminded abt it..hata cjui ilikuwaje mpaka jamaa hakushtuka!....ila mwaka wa nne!!!!!!!!!!!...daaah!!!
inaonyesha wazi kama sheria hiyo na adhabu yake anaijua coz alianza nayo tangia 1st year! Perhapes seemz tz unfortutanet!
Ushauri:aappeal against senate judgment
 
kama kisa ni simu pekee inawezekana walikuta amendika nondo humo ndani
simu za sasa zina microsoft office unasave karibu desa zima..
nadhani hajatimuliwa bila kupewa haki ya kujitetea
na hata hivo ana right to appeal amtafute lawyer..


Upande mwingine.walimu wa vyuo kutwa kucha kukomoa wanafunzi kwa kuwafelisha
wanashinda kupika majungu hata paper hawapublish licha ya kupenda ngono kwa wanafunzi.
hata waliosoma nje bado wakirudi yanakua yaleyale..
vyuo vimekosa sifa kwa sababu ya ufundishaji wao mbovu na tabia zao.
 
Ukipewa booklet chuo cha UDSM mbele kuna masharti na moja linasema simu za mkononi haziruhusiwi kuingizwa ndani ya chumba cha mtihani.

Ukiingia nayo hata kama ipo off,haijalishi ina uwezo wa kufungua word or pdf docs au aina,kinanuka! kama alikamatwa nayo basi tena b'se it is taken as a part of cheating.

Na huwa kuna form maalumu ambayo inajazwa na mashahidi na mwanafunzi aliyehusika hutakiwa kukubali/kukataa kosa na kuweka signature,form huambatanishwa na uthibitisho.

Hata akikata rufaa,kama kwenye form alikubali kuwa alikutwa na simu...

Huyo atasubiri sana!! Nampa pole tu.
 
senate ipo sahihi kabisa kwasababu hata kabla paper haijaanza wanasisitiza sana kuhusu simu lkn nadhani hakujali na hakujua ndio 40 yake.....yeye si wa kwanza nilishaona jamaa wengi tu wakirudi mwaka kwa kukutwa na simu kwny chumba cha mtihani kilicho waisaidia ni simu kukutwa imezimwa,hivyo wakapata cha kujitetea.ajaribu chuo kingine akamalizie lkn siamini kama appeal huwa zinashinda pale UD
 
Mara ngapi kaka unasoma yale maelekezo smtmz ni kupitiwa pressure za mitihani mamo kama hayo ww unafikiri tangu 1st year to 4 th year alikua hajui hzo sheria? mpaka akaja kuingia nayo kwenye mtihani?? Jamaa mwenyewe cku hyo tulikua na mitihani miwili mmoja sa 5b na mwingne a 11 jioni anadai asubuh kabla ya kuaj kwenye mtihani alipigiwa sim kutoka kwao kua mama yake ni mgonjwa sana afu na ukufikiria ratiba yenyewe ya mtihani ilivyokua imekaa jamaa akaamuakubeba cmu kwa ajili ya kua anawasiliana nao home kwao kujua hali ya mama yake bt bahati mbaya ndo ivyo akaingia nayo kwenye mtihani bila kujua
 
kuna wengine pia 10 wamekutwa na cmu nao pia zilikua zmezmwa ilani miaka ya chini nao wamewadisco pia yaaan hata cjui wameangalia nn
 
kuna wengine pia 10 wamekutwa na cmu nao pia zilikua zmezmwa ilani miaka ya chini nao wamewadisco pia yaaan hata cjui wameangalia nn

Wengi huwa tunachukulia poa ila ukitaka kujua ni wkt gani UDSM huwa ipo serious, haribu kwenye mitihani.
 
Akubali matokeo na kutafuta jinsi nyingine ya kuendelea na maisha.
 
"Our greatest glory is not in never falling, but in rising every time we fall." - Confucius.
it was never meant to be.
he/she has to move on
it doesnt mean the end of life.
it just means his/her part of the story at UDSM is over and this event marks the beginning of a completely new journey.
encourage him/her to be STRONG and never to lose HOPE for God is GOOD............ALL THE TIME
 
Dah!kuna mwingne 1st year alikua anasoma sheria,nae alikutwa na cmu kama huyo mshkaji.na yeye wamempga disco aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…