USHAURI DOCTORS:Huyu mama kashika ujauzito akiwa na mshono miezi 11(alijifungua kwa operation c-section)

USHAURI DOCTORS:Huyu mama kashika ujauzito akiwa na mshono miezi 11(alijifungua kwa operation c-section)

Heri wewe ana miezi 11, kuna mmoja alipata baada ya miezi 3 na still akazaa vizuri kwa operation ya pili ndani ya miezi 12.
duuuh hata nae anadai doctor kamwambia afadhali ya yeye nashukuru sana
 
Usimfanyie hivyo mwenzio ..

Tumia njia za uzazi wa mpango, zaa kistaharabu.
 
Mleta mada next time mtumie uzazi wa mpango uwe na huruma kwa mkeo, though atazaa salama ila kwa operation na inabidi awe karibu na Dr ili awahishwe operation. Namhuhurumia huyo mama operation inauma balaa maana kidonda kwa ndani kinachukua two years had kupona tena kwa wafanya mazoezi. Nyie kuwe karibu na ma gyno had atakapojifungua
Asante sana mkuu nashukuru kiukweli ushauri umemtuliza natanguliza shukrani mkuu
 
Usimfanyie hivyo mwenzio ..

Tumia njia za uzazi wa mpango, zaa kistaharabu.
Wanazikimbia ujue mkuu kama umeoa hata mimi binafsi situmii labda kama kuna njia isiyo na madhara ipi hiyo niingie pia maana nimeshuhudia live kwa wenzangu wake zao wakikosa period hadi kupata uvimbe wa kizazi
 
Atajifungua tu mkuu! Kwa sasa aendelee kunyonyesha mpk anapokaribia kujifungua ila akae karibu na hosp na awe anamwona daktari mara kwa mara. Hiyo ilishawahi kunikuta
huenda ilikukuta ukiwa umekuza mtoto mkuu miezi 11 michache sana
 
Asante sana mkuu nashukuru kiukweli ushauri umemtuliza natanguliza shukrani mkuu
Mtoto mtapata vzuri kabisa maana hyo ni karibia mwaka though kidonda hakijapona vzuri. Jitahidini awe karibu na dr na asisubirishwe had uchungu umpate maana inaweza kuleta uterus Ku rupture mkuu. Yote msisahau maombi ni muhimu all the best kwenye kusubiria baraka ya kichanga.
 
Amen na asante sana mkuu nashukuru sana kadai hata doctor kamsahuri hivyo asisubirie uchungu kwa afya yake thanks sana imemfikia
 
Wanazikimbia ujue mkuu kama umeoa hata mimi binafsi situmii labda kama kuna njia isiyo na madhara ipi hiyo niingie pia maana nimeshuhudia live kwa wenzangu wake zao wakikosa period hadi kupata uvimbe wa kizazi

Zipo njia nyingi, waendee wataalamu wa afya wata kusaidia ipi ni njia bora ya kupanga uzazi.

Kuna watu wachache wajinga wanapotosha kuhusu uzazi wa mpango, msiwasikilize.

Waoneni wataalamu wa afya.
 
Itabidi nijitume niwafuate pia maana unachokiona mtaani hadi unaona ujiunge kundi la wasiotumia maana yaonyesha madhara makubwa Kwa wanaotumia TUPUNGUZE KESI KABLA HATUNYOLEWA
Zipo njia nyingi, waendee wataalamu wa afya wata kusaidia ipi ni njia bora ya kupanga uzazi.

Kuna watu wachache wajinga wanapotosha kuhusu uzazi wa mpango, msiwasikilize.

Waoneni wataalamu wa afya.
 
Nenda kwa Gynocologist atakusaidia....
Hii kitu hutokeaga mama kama ananyonesha na hapati siku zake huwa mistake hii hutokeaga sana na ukija kistuka utakuta 2 inaelekea mi3
 
gynaecologist: mtaalamu wa afya anayehusika na huduma au matibabu kwa wanawake hususani yanayohisiana na mfumo wa uzazi.

Obstetrician: mtaalamu wa afya anayehusika na maswala yote yanahusu mimba tangu utungishwaji mpaka mtoto anapozaliwa,au jambo lolote linalohusiana na mimba kwa upande wa mwanamke.

Hii ni nyongeza tu, kwa baada ya kuona recommendations za kuonana na gynaecologist
 
Back
Top Bottom