Ushauri: Dr Ayub Ryoba awe Msemaji Mkuu wa Serikali, Salim Kikeke awe Mkurugenzi Mkuu TBC

Ramli Chonganishi.
 
Dr Ryoba ana uelewa mkubwa wa mambo mbalimbali ya nchi hii, hivyo angetufaa zaidi kwenye usemaji wa serikali hasa kipindi hiki ambacho wananchi hawamuelewi mama kwa sababu tu wamekosa taarifa jinsi maendeleo yanavyoenda.
Kwa Kikeke bado aendelee kulelewa ndani ya utumishi kama azina ya miaka ijayo
 
Kwahiyo MAMA analeta maendeleo, hayaonekani ila inabidi watu waelezewe ili wayaelewe?
Kwamba Watu hawajui Sukari imetoka 1500 mpaka 4500 kipindi cha mama tunataka mtu aje kutuelezea "huko si kupanda ni kushuka ?"

Kwamba Sementi imetoka 15,000/- mpaka 18500 tunataka Mtu aje kujieleza?
Kwamba hakukuwa na tozo, sasa zimewekwa hata kwenda chooni unalipia tunahitaji mtu aje kutuelezea.?
Kwamba , Ripoti ya Ufisadi CAG hakuna hatua yeyote kwa waliotajawa na kila siku watu wanahamishwa vitengo tofauti na kipindi cha Jiwe walau alikuwa anafukuza wawili watatu , tunahitaji Ryoba aje kutuelimisha?


# Elimu elimu elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…