Ushauri: Engine ya gari inatetemeka na kuunguruma sana

True Lover

Member
Joined
Aug 8, 2016
Posts
32
Reaction score
47
Wakuu wasalaam!

Ninaombeni ushauri, nina gari Rav4 kill time, engen yake naambiwa ni ile kubwa inanisumbua kwa kutetemeka na kunguruma sana. pia inanishinda kwa inavyokula petroli kulingana na pato langu, Hapa nawaza ninunue engen mpya vvti ya cc 1290 ile ya ist, je itafaa (itaingiliana)? na inaweza patikana kwa bei gani at minimum? Ninaomnbeni msaada na ushauri wa ziada wataalamu wangu.
 
Kwanza Engen ni jina la kampuni ya mafuta,
Ni either useme Engine kwa kiengereza au Injini kwa kiswahili,
Pili sikushauri uweke hiyo Injini, sana sana labda uweke 1ZZ ile ye CC 1,790 lakini utahitajika kubadili na Gearbox yake pia
 
Nashukuru kwa marekebisho,nlimaanisha Engine. sababu kubwa ni kutaka minimum consuption as posible, ikifika cc1,790 naona kama nimerudi kulekule maana ya sasa ni cc 1998. Unadhani kuna gap wapi nikiweka hii ndogo?
 
Mkuu kila Ukubwa wa gari na Injini yake,
Lakini pia kuna vitu kama nafasi ya Injini kukaa kwenye gari pia uelekeo na wa Injini,
Sio kila Injini inaenea kwenye kila Gari,
Pili Injini inaweza kuenea lakini uelekeo wa Vifaa vingine Kama Engine Mounting, Propeller, etc vikapishana
 
ahsante sana mkuu, umenifungua mtazamo. nimepata pa kuanzia
 
ahsante sana mkuu, umenifungua mtazamo. nimepata pa kuanzia
Yaani mki nachojua kwa kawaida Rav4 zina injini za aina mbili tu,
Hiyo unayotoa (1AZ) cc 1990 na 1ZZ c1790,

Ila sasa kibongo bongo kama wanaweza kukuwekea Injini ya Toyota kwenye Pajero IO au Landrover Freelander basi hata hiyo plan yako inaweza kufanikiwa Mkuu wangu,
Jaribu kuwacheki tu
 
Hiyo itakuwa ni engine ya D-4 1998 ulaji wake wa mafuta ni mkubwa mno tofauti na VVTI-1790 nakushauri iuze hiyo gari uweze kununua gari ndogo kutokana na pato lako
Ahsante kwa ushauri mkuu, Ni kweli injini yangu ndo D-4 1998 na gari bado naipenda maana nakaa vijijini sana so sitaweza kutumia gari za chini, SO HILI WAZO LA KUWEKA VVTI YA CC 1,290 LINGEFAA INGEKUWA POA SANA.
 
Injini inatetemeka unapowasha gari au? Embu jaribu kucheki mounting, hasa ile iliyo chini ya engine inawezekana imekatika.
YES,NINAPOWASHA GARI INJINI INATETEMEKA, NA KUNA FUNDI KANIAMBIA TATIZO LITAKUWA mounting LAKINI KWA SASA SIJATAKA KUSHUDHULIKIA MAANA SHIDA YANGU KUBWA NI CONSUPTION
 
YES,NINAPOWASHA GARI INJINI INATETEMEKA, NA KUNA FUNDI KANIAMBIA TATIZO LITAKUWA mounting LAKINI KWA SASA SIJATAKA KUSHUDHULIKIA MAANA SHIDA YANGU KUBWA NI CONSUPTION

MWANZONI NILIKUWA NAKAA TOWN KARIBU NA NINAPOFANYIA KAZI,LAKINI SAHIVI NIMEHAMIA KWANGU AMBAKO NI MBALI KUTOKA MJINI NA HAMNA LAMI SO KWA GARI YA CHINI NITAKUWA NAKWAMA SANA,SO LIKAJA WAZO LA KUBAKI NA GARI YANGU BUT NIBADILI INJINI YENYE LESS CONSUPTION.
 
Uza hiyo nunu Terious. Au Cami
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada, hii inshu ya kununua engine ya gari aina fulani kufunga gari aina nyingine, naona ni mateso makubwa na usumbufu usio na maana wala faida, jichange nunua gari yako ndani ya uwezo wako kiuchumi achana kabisa na gari za kuungaunga zitakutia umasikuni.
 
NOTED MKUU
 
Hiyo itakuwa ni engine ya D-4 1998 ulaji wake wa mafuta ni mkubwa mno tofauti na VVTI-1790 nakushauri iuze hiyo gari uweze kununua gari ndogo kutokana na pato lako
VVTI cc 1790 naipenda hii injini mafuta ya elfu 10 siku nne home to work
 
Kwanza tutibu kutetemeka kwa injini jaribu kuangalia injini mounting yawezekana kwa ndani kuna mpasuko so karibu ikatike au imepishana, ila kama ni kama ni kubadili injini mpya basi usitake modifications huwa baadae inakuja kusumbua sana funga IZZc1790 kama unataka kuendelea kutumia gari yako
 
thanks mkuu kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…