llakini ipatikane namna ya kuelimisha watoto kuhusu hii ishu kwasababu walawiti wengi ni watu wazima, wanawadanganya watoto na vitu vidogo kama chipsi na pipi....
Kuwaelimisha watoto sio suluhu. Watoto wana behave in their natural form. Huwezi mkataza mtoto asisalimie watu au asiongee na watu sababu kuna wabakaji.
Dawa ni kubaini na kuwaprofile hawa pedophiles sababu tabia za pedophile zinajulikana na ni rahisi sana kuwakamata.
Nadhani jamii iwe na utamaduni wa kuwachunguza watu. Unapishana na mtu fulani unamjua wa mtaani anapita na mtoto wa fulani unasema mimi hayanihusu. Angekuwa ni mtoto wako ungepishana nae wanaelekea sehemu na mtu mzima ambaye hauna mazoea nae ya kusogelea watoto wako.
Nadhani hapo dhamira iwekwe kwenye kuwabaini watu wenye tabia za hovyo. Wanajamii wapate elimu kupitia mitandao ya kijamii ya tabia za watu ambao wanafanya haya matendo.
Mimi mbona naweza mshtukia mtu wa hivyo mapema sana sababu atakuwa anaonyesha kuwa na interests za ziada kwa watoto anataka kuwatarget.
Imagine mtu anaingiaje na mtoto mdogo na kujifungia nae ndani akisema wanatazama video bila mzazi wake kujua.
Au mtu anakuwaje busy na mtoto wa mtu na kwenda nae mbali mazingira ambayo si sawa kuwa na mtoto wa mtu.
Kama unapenda watoto fanya katika mazingira ambayo ni salama na ya kuaminika.
Na wazazi wasiwe comfortable sana kumuacha mtoto unasema yupo na mtu fulani siku nzima hata hujui mtoto yupo wapi. Ni vema kutrack movements za mtoto na kujua yupo wapi na yupo na nani wakati wote.
Pia kuna watoto ambao huwa wanapata early puberty especially watoto wa kike. Hawa watoto wanakuwa na tabia ambazo huwa zinawavutia sana hawa pedophiles sababu wanawarahishia kazi ya kutengeneza mazingira ya kuwabaka. Ni vema kumtathimini mtoto wako ukiona ameanza kupevuka mapema then umshape tabia ili asije kosea mwenendo akaangukia kwenye mikono ya hawa mabazazi.