Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Mwenyekiti mpya wa CHADEMA ameshatoa masharti ya nyie kurejea kwenye chama chake. Masharti hayo ni magumu na hata kama mtarejea CHADEMA, hakuna uwezekano wa nyie kuwa wagombea wa ubunge wa majimbo wala wa viti maalum. Mtabaki kuwa wanachama wa kawaida tena chini ya uangalizi maalum kama alivyotamka huyo mwenyekiti mpya. Vipaji vyenu vitakuwa vimehitimishwa.
Nchi yetu inatambua vipaji vyenu na michango yenu makini yenye busara ya kuikosoa na kuirekebishs serikali kipindi chote mlichokuwa upande wa upinzani. Taifa lilifaidika sana kwa michango yenu hiyo na lingependa muendelee kwa nafasi hizo.
Hivyo basi tunawashauri muhamie chama cha kijana mwenzenu makini na mzalendo cha ACT ili mkagombee ubunge wa majimbo au wa viti maalum kupitia chama hicho. Tuna uhakika mkifanya hivyo mtaendelea kuwa wabunge na sisi kuendelea kufaidia na michango yenu ya kistaarabu ya kuikosoa na kuirekebisha serikali yetu kwa manufaa yetu sote.
Pia soma=> Halima Mdee na Wenzake 18 walifukuzwa CHADEMA kwa Usaliti, Nafasi yao Haipo tena na haitokuja kuwepo
Nyie hamtakuwa wa kwanza kufanya hivyo. Maalim Seifu Hamad Sherifu alifanya hivyo na timu yake baada ya kuvurugana na Lipumba huko CUF. Hivyo ingalipendeza hata wale waliokuwa timu Mbowe wakang'oa nanga na kujiunga na ACT wazalendo.
Tungalipenda Zitto Kabwe akawa mbunge na KUB ajaye. Tungependa kuwa na chama kikuu cha upinzani kingine huku Tanzania bara kikichuana kushika dola badala ya hiki kimoja cha chadema kinachodharau vyama vingine na kuviita CCM B. Ni muda mwafaka sasa watu kama Bony Yai, Mrema, Kagaila, Wenje, Yericco na wengine wenye wa aina hiyo wakajiunga na kuimarisha ACT wazalendo.