Pre GE2025 Ushauri: Halima Mdee na wenzake 18 taifa letu bado linahitaji michango yao ya hekima, busara na ustaarabu wa kuikosoa serikali yetu. Wajiunge ACT

Pre GE2025 Ushauri: Halima Mdee na wenzake 18 taifa letu bado linahitaji michango yao ya hekima, busara na ustaarabu wa kuikosoa serikali yetu. Wajiunge ACT

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hao wanawake ni wabobevu kwenye siasa,hivi karibuni watatangaza wanaenda wapi,subiri tu
Swali kuu alilouliza Lisu litawaandama kokote waendapo. Wajitulilie wasubiri ukuu wa wilaya, na teuzi zingine toka kwa aliewafadhiri huo ubunge
 
Mwenyekiti mpya wa CHADEMA ameshatoa masharti ya nyie kurejea kwenye chama chake. Masharti hayo ni magumu na hata kama mtarejea CHADEMA, hakuna uwezekano wa nyie kuwa wagombea wa ubunge wa majimbo wala wa viti maalum. Mtabaki kuwa wanachama wa kawaida tena chini ya uangalizi maalum kama alivyotamka huyo mwenyekiti mpya. Vipaji vyenu vitakuwa vimehitimishwa.

Nchi yetu inatambua vipaji vyenu na michango yenu makini yenye busara ya kuikosoa na kuirekebishs serikali kipindi chote mlichokuwa upande wa upinzani. Taifa lilifaidika sana kwa michango yenu hiyo na lingependa muendelee kwa nafasi hizo.

Hivyo basi tunawashauri muhamie chama cha kijana mwenzenu makini na mzalendo cha ACT ili mkagombee ubunge wa majimbo au wa viti maalum kupitia chama hicho. Tuna uhakika mkifanya hivyo mtaendelea kuwa wabunge na sisi kuendelea kufaidia na michango yenu ya kistaarabu ya kuikosoa na kuirekebisha serikali yetu kwa manufaa yetu sote.

Pia soma=> Halima Mdee na Wenzake 18 walifukuzwa CHADEMA kwa Usaliti, Nafasi yao Haipo tena na haitokuja kuwepo

Nyie hamtakuwa wa kwanza kufanya hivyo. Maalim Seifu Hamad Sherifu alifanya hivyo na timu yake baada ya kuvurugana na Lipumba huko CUF. Hivyo ingalipendeza hata wale waliokuwa timu Mbowe wakang'oa nanga na kujiunga na ACT wazalendo.

Tungalipenda Zitto Kabwe akawa mbunge na KUB ajaye. Tungependa kuwa na chama kikuu cha upinzani kingine huku Tanzania bara kikichuana kushika dola badala ya hiki kimoja cha chadema kinachodharau vyama vingine na kuviita CCM B. Ni muda mwafaka sasa watu kama Bony Yai, Mrema, Kagaila, Wenje, Yericco na wengine wenye wa aina hiyo wakajiunga na kuimarisha ACT wazalendo.
Waende tu hata CCM sisi tulishamalizana nao kitambo sana
 
Kwan wao ndio wanasiasa pekee wa kike ambao wapo Tanzania,hatuna wengine ambao wapo vizuri? Hawa ni wachumia tumbo achaneni nao.
 
Sidhani kama umefikiria vizuri kuhusu dhana ya kiongozi wa wananchi. Kwenye hilo uadilifu ni nguzo namba moja. Asiye mwadilifu, hafai kuwa kiongozi.

Kwenye sakata la Mdee na wenzake, limelemea zaidi kwenye kukosa uadilifu na kufanya udanganyifu. Kwa ujumla nchi yetu inahitaji viongozi waadilifu.

Kwa tafsiri hii, tunapaswa kuachana na akina Mdee, kama wananchi. Nchi yetu inao akina Mdee wengi sana ambao ni waadilifu, huwaoni kwa kuwa akina Mdee wameziba nafasi.

Ova
Wewe ndiye ulitakiwa uitwe Dr. halafu huyo muanzisha uzi aitwe kilaza Akili.
Kongole sana.
Uadilifu ni nguzo kubwa ya uongozi.
 
Milango iko mingi. Huko chadema mumewafungia mlango. Tatizo liko wapi kama watatumia mlango wa ACT ambao uko wazi kwao. Kura za wananchi ndizo zitakazoamua kama waendelee na ubunge majimboni kwao au ubunge wa viti maalumu. Kwani ni lazima wawe chadema ili kuendelea kufanya siasa.? Upende usipende, kilichotokea huko chadema 21 January 2025 ACT na CCM kitawanufaisha sana kwenye uchaguzi mkuu wa October 2025. Kwanza hii chadema ya Tundu Lissu haitashiriki kwenye uchaguzi huo kwani hakutakuwa na hiyo reform wanayoitaka. Kuzuia uchaguzi hawana ubavu huo wa kupambana na akina Afande Mulilo etc. Hivyo ni obvious kwamba ACT wazalendo ndiyo itaibuka kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni na Zitto Kabwe kuwa KUB. Chadema itabaki kuwa chama cha wanaharakati.
Kuna mahali nadhani unashindwa kunielewa, na kwa sababu mimi nimetoa maoni kwa nafasi yangu ya mwananchi, Mtanzania.

Nawe, naona umetoa maoni kama shabiki wa Mdee na wenzake. Na kwa bahati mbaya masuala yanayohusu nchi hayataki ushabiki bali uhalisia.

Unajua ukijumlisha malipo yao ya jumla kwa Ubunge wao haramu kwa kipindi cha miaka mitano ni karibia bilioni 5 x 19?

Huwa siko kwenye ushabiki katika masuala yanayohusu nchi yangu. Kwani hakuna eneo jingine duniani naweza kuita ni nchi yangu ya asili.

Ova
 
Hao akina Yericko uliowataja ndio waliokuwa wanaongea kwa kejeli wakiamini Mbowe atamshinda Lisu, kwamba mkishindwa hakuna kuhama chama, sasa naona unataka wameze matapishi yao. Hao covod 19 lini mlianza kuwaona ni wa maana? Na huko ACT unakotaka waende hakuna wagombea wengine, wako wanasubiri wasaka madaraka waje wawape nafasi?

Huu upuuzi wa kusubiri wasaka madaraka walikosea cdm uchaguzi wa 2015, wakapokea wahamiaji haramu toka ccm, matokeo yake wengi wa hao wahamiaji haramu ndio walirejea ccm kuunga ile project chafu ya kuunga mkono juhudi. Unadhani ACT hawajui upuuzi huo?

2015 ni kesi nyengine kabisa, lowasa alitoka CCM, hapa tunazungumzia vyama vya upinzani
 
Tatizo hao wote uliowataja kwenda ACT, sio maarufu kisiasa, hawana influence, yaani sio mtaji kisiasa, so hawana impact kokote kule wakienda, wao pia wanajua

Usajili wa uhakika wa ACT ni Mbowe , hao wengine ni jalizia tu
 
Snitch hata siku moja hajawahi kua na uchungu na TAIFA lake zadi ya tumbo lake.
Taliban's wangewapiga chuma live.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom