Ushauri - Hospitali ya kujifungulia

Ramthods

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2009
Posts
515
Reaction score
187
Wadau,

Mimi na mwenza wangu tunatarajia kupata mtoto wetu wa kwanza mwishoni wa April, au mwanzoni nwa May Mungu akijalia.

Kwa sasa mama anafanyia clinics pale Marie Stopes, Mwenge. Hatuna insurance, so nalipa toka mfukoni.

Nimefikiria kuwa ajifungulie pale pale, lakini sina uhakika sana kama ni pazuri, ukichukulia huyu ndio mtoto wa kwanza, so sina kabisa uzoefu.

Nimejaribu kucheki gharama za AghaKhan, ila naona zipo juu sana. Kwa mfano, kama ikitokea akajifungua kwa operation, basi gharama ni kama Mil 4 kasoro kidogo.

I would be confortable paying somewhere around 1.5Mil kwa kila kitu.

Ningefurahi sana kama ningepata ushauri wowote toka kwa wadau wenye uzoefu kuhusu uchaguzi wa hospitali.

Asanteni sana.

Ram
 

Ningekushauri mtafute hosp ya serikali,wana madhaifu yao lakini ndo mahalo mtapata huduma.za uhakika.private hosp nyingi wapo after money...utaambiwa mtoto katanguliza makalio ili ufanyiwe operation tu wakati mtoto kakaa fresh tu

Ni ushauri tu
 
Binafsi nakushauri muende hospitali za serikali ndio ziko vizuri katika masuala haya, japokuwa wana changamoto mbali mbali ila wanafaa sana.

Kuna ndugu yangu mmoja hakutaka kujifungulia serikalini akaenda agakani, kilicho tokea ni kwamba, alifanikiwa kujifungua lakini ikagundulika kuwa mtoto anahitajia akae kwenye joto kwa siku kadhaa, wakamwambia aende serikalini apate hiyo huduma, alipokwenda serikalini wakamzingua kama masaa kadhaa hivi bila kumhudumia.

Kwa upande wangu, nawashauri mtumie hosp. Za serikali mfano mwananyamala (kuna mtu amejifungua hapo kwa oparesheni na ametumia laki mbili na kidogo napo ni baada ya kuona njia ya uzazi wa kawaida inashindikana).

Ni hayo tu ndugu.
 
Nimejaribu kucheki gharama za AghaKhan, ila naona zipo juu sana. Kwa mfano, kama ikitokea akajifungua kwa operation, basi gharama ni kama Mil 4 kasoro kidogo.

Kuna dalili zozote unaziona zinaweza kupelekea akajifungua kwa operation?
 
Wazazi mna hofu sana siku hizi na wenye hospitali binafsi wanaitumia hofu hiyo kujinufaisha.
Mpeleke hospitali za serikali tu na atajifungua vizuri kwa gharama ndogo tu na hata kama ni operation atafanyiwa ikibidi.
 
Kama inawezekana kafanye vopimo vya abdominal ultrasound ili kujua mtoto kalala vip katanguliza nn na ana umri gani

Kama vipimo vitakuwa safi tegemea mkeo kujifungua salama kabisa na mtumishi yeyeto mwenye fani ya afya aweza kumsaidia popote tu na akajifungua vzr sana

. licha ya kuwa anatakiwa kuhudhuria klinic zote kwa afya nzuri ya uzazi.

Tunapendelea sana mimba ya nzao ya kwanza ajifungulie hospitalini for complication reduction.
 
Kwa sasa hakuna complication yoyote ambayo inaweza pelekea kuhitaji operation

Basi usihofu, mpeleke hospitali yeyote ya serikali mwananyamala au temeke ila usisahau kumpa nesi elfu 10 tu (ya nauli au maji ya kunywa) atamshughulikia kama ndugu yake kabisa.
 
Acha woga miela yote ya nini hiyo, nenda kajikunje mwenyew hospitali za serikali.
 
Uzazi mwingine, jitahidi kufanya maamuzi mapema ya mahali pakujifungulia ili muweze kuhudhuria kliniki mahali hapo. Inasaidia sana kwasababu mazingira mnakuwa mnayafahamu na maendeleo yenu wanakuwa nayo katika kumbukumbu zao.. Kila la kheri.. Mungu atawasaidia, mtajifungua salama.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Mpeleke muhimbili kuna huduma ya private pale hata kwa clinic ni nzur sana unapata daktari wako na huduma ni very affordable.
pia pale hata mzazi akiwa na complication yoyote ni rahisi kupata huduma
 
Basi usihofu, mpeleke hospitali yeyote ya serikali mwananyamala au temeke ila usisahau kumpa nesi elfu 10 tu (ya nauli au maji ya kunywa) atamshughulikia kama ndugu yake kabisa.

Huu ndio ushauri wa mwisho na ulivyomalizia ndio habar ya mjini usipo mpa tuuu utaona, na kingine serikar hospt wa mama wajawazito kujifungu kawaida au operation ni bure kabisaaaaa...
 

Hayo yote ulio sema yanaweza yakawa safi lakini siku ya siku ikaonekana njia ya uzazi ndogo.
 
Yaani mkuu nenda kote but gvt hosp ndo uhakika...wakikupiga kisu ujue imeshindikana natural way mtoto anataka kutokea dirishani baada ya mlangoni so jiandaeni kwa utundu...just joke..

me nimejifungua gvt hosp na nimepata huduma nzuri tu.....nilienda saa kumi usiku,saa nne asubuhi.nimejifungua saa kumi jioni nimeruhusiwa very safe and health....mtegemee Mungu sawaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…