Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwa mtazamo wangu, tunapotaka kuimarisha umoja miongoni mwa vyama vya upinzani nchini, moja ya jambo tunalopaswa kuliepuka au kutoendelea nalo ni kuita CHADEMA chama kikuu cha upinzani.
Nasema hivi kwasababu, matmuzi ya jina hilo yanajenga inferiority complex miongoni mwa vyama vya upinzani na pia matumizi ya neno hilo yanachangia upinzani miongoni mwa vyama vya upinzani badala ya umoja.
Ni wazi matumizi ya maneno chama kikuu cha upinzani yametafsiriwa kutoka kwenye matumizi ya maneno: "main opposition party " yanayotumika katika lugha ya kingereza. Swali ni je, kwa lugha ya wenzetu, neno "main" linaleeta tafsiri kama inayoletwa na maneno chama kkuu? Na je, tunapaswa kuiga kila kitu?
Binafsi naona maneno sahihi ni kama chama kikubwa cha upinzani au chama chenye wafuasi wengi na si maneno chama kikuu.
Mimi ni mpenzi CHADEMA lakini huwa sipendezwi na matumizi ya hayo maneno kama ambavyo huwa sipendezwi na matumizi ya neno "mtukufu" unapotaka kum-address kiongozi na ni bora watu wengine ambao sio wana-CHADEMA au viongozi wa CHADEMA ndio wakatuita hivyo lakini sio sisi WANA-CHADEMA na viongozi wetu.
Let's be humble na tuachane na huu "ukuu" kwani nguvu ya chama chetu inajieleza yenyewe.
Nafarijika sana leo kuona vyama vingine vya upinzani vikitoa mawakili wao kuungana na wale wa CHADEMA kumpigania kamanda Mbowe ingawa vyama hivi sometimes huwa vinatupa wasiwasi ila adui yetu mkubwa ni CCM na si ACT, NCCR au chama kingine chochote cha upinzani.
Ni ushauri kwa nia njema.