Ushauri: Iundwe Kamati huru kubaini chanzo cha nyufa JNHP maana kuna harufu ya uhujumu uchumi

Walibya wanadai walipigia kelele serikali, japo serikali ziko mbili lakini hakuna aliyejali. Sisi wenye serikali moja ndio kwanza tutawapiga marufuki watu kuripoti taarifa za nyufa.
Lengo la Mradi kuwa white elephant litimie...! Hii hujuma itatengenezewa" firing squad" ikidhibitika ni hujuma kweli!!
 
Maji yananguvu balaa usicheza na maji kama kunanyufa baaassiiii mradi wooteee ni buureeee bilivu Mii!!!
Hiyo itakuwa ni hujuma kama ni kweli ! Kwani waliotengeneza hilo bwawa wanasemaje kuhusu bwawa kuweka nyufa ???!! Duh 🙄 hatar sana !!!
 
Eeehh nyufa wakati ujenzi unaendelea, kuna thread hapa niliona two weeks ago kuhusu hizo nyufa nikaapuuza, kumbe ni kweli? Basi mkandarasi ahojiwe vya kutosha
Tena hiyo inamuhusu moja kwa moja mkandarasi ! Wahojiwe waeleze sababu ya hizo nyufa ni nini ??!
 
Mungu saidia bwawa lipasuke siku viongozi wote wakuu wakienda kulitembelea tena wasombwe na maji maiti zao zikutwe hata juu ya vichaka vya miba waaibike na familia zao
 
Tumeona Naibu waziri mkuu, Mh Dotto Biteko akifanya ziara katika Bwawa la Mwalimu Nyerere na Kutoa ushauri jinsi ya kuziba nyufa zilizoanza kuonekana kwenye ukuta wa Bwawa
Mada ni nzuri sana sana ila kwanini Biteko NDIO atoe ushauri wa kitaalam Kwa wataalam??
 
Yupo Hadi sasa wizara ya Mambo ya nje kama vile hakipo kilichotokea.

Kuna mdau alisema kuteuliwa Biteko ni kuangushiwa jumba bovu, naanza kuliona,

Maana Badala ya kujiuliza Hali hiyo inefikaje hapo,

Anageuka mshauri wa kuziba nyufa.
Biteko ndio anaekamilisha desert mission yaweza KUWA ndie FDR ajaye!!
 
Mkandarasi na mshauri wanasemaje? Muda wa matazamio , umeisha?
 
Mada ni nzuri sana sana ila kwanini Biteko NDIO atoe ushauri wa kitaalam Kwa wataalam??
Hilo ndilo jambo linalotupa hamaki,

Kwanini hajiulizi chanzo ni nini, Ili kutafuta suluhu ya kudumu!!

Ni kama katumwa kumtuliza mambo yalovurugika.

Hatutakubali.
 
Sawa kabisa
 
kuna kipindi waziri kalemani alionekana kwenye tv akimlalamikia mkandarasi kwa kujenga chini ya Kiwango kwa kujenga nguzo chache kwenye ukuta wa bwawa tofauti na inavyotakiwa na kuweka wasimamizi wataalamu wachache .
 
Limechakaa kabla ya kutumika🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
kuna kipindi waziri kalemani alionekana kwenye tv akimlalamikia mkandarasi kwa kujenga chini ya Kiwango kwa kujenga nguzo chache kwenye ukuta wa bwawa tofauti na inavyotakiwa na kuweka wasimamizi wataalamu wachache .
Kwani mkataba inasemaje mkandarasi akijenga chini ya viwango vinavyohitajika ??!
Ni lazima mkandarasi awajibike kama wanavyowajibika wakandarasi wengine wa barabara na miradi mingineyo !!
Masharti ya kuwajibika ni lazima yatakuwepo kwenye mkataba !!
 
Mada inashauri uchunguzi ufanyike kubaini tatizo, haisemi nani alaumiwe Kwa nyufa zilizojitokeza.
Watakaofanya uchunguzi ni sehemu ya watakaotoa maamuzi ya hatua za kuchukuliwa. Maamuzi yatafanyika kuendana na taswira ya chama kuelekea uchaguzi wa 2025. Hakuna maamuzi au hatua za maana zitachukuliwa nje ya utashi wa kisiasa.
 
Nilipomsikia mama akilalamika kuhusu ongezeko la bei ya ndege mpaka akawaita stupid na kuagiza watupishe, lakini hadi leo hawajawahi kutupisha,ndipo nilipoolewa kuwa mafisadi wana nguvu kuliko.
Na ndio wanahamua nchini iendeswe vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…