ufumawicha
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 504
- 209
Jamani nimebahatika kupata ka sh 350,000 sasa kuna mtu kanishauri nianze taratibu kununua mitumba na kuiuza.Msaada wa mawazo please.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani nimebahatika kupata ka sh 350,000 sasa kuna mtu kanishauri nianze taratibu kununua mitumba na kuiuza.Msaada wa mawazo please.
Watu wengine hawachangii labda kwa sabb wanaona hiyo hela ni ndogo, mchango wangu ni hivi.
1.Huyo mtu amekushauri lakini je ww uko tayari na biashara hiyo? kumbuka sifa ya kwanza kuliko zote katika ujasiliamali ni upendo wa biashara usika. ni lazima uipende biashara yako ndipo upate mawazo mapana zaid.
2. Sifa ya pili ni kuifaham, unatakiwa kuijua hiyo biashara yako. hii unaweza kufanya kama mchangiaj mwenzangu alivyo kuelekeza nenda ufanye utafiti ujue wenzio wanafanyaje?
3.Sifa ya tatu ni ujasili, hakikisha ukiamua kuifanya hiyo biashara, ukaipenda, ukaijua,hakikisha sasa unakuwa na moyo wa ujasili yaani moyo wa kukubaliana na changamoto zake. hepuka neno matatizo, ukiona matatizo utashindwa ila ukion kuwa ni changamoto tu utazitafutia njia mbadala.
4.Kwa huo mtaji usinunue mitumba ya jumla yaani zilizo fungwa. nenda kwa wale wanao nunua bei ya jumla wakifungua ww changua nguo moja moja zenye quality.
5.Kama ni nguo za kike tembeza sehemu ambaka unaweza kuwakuta wanawake zaid ya 2-3 kwa pamoja,mfano kwenye saloon za kike lazima utawakuta tu. na pia unaweza kwenda sehemu za chuo kikuu au popote penye chuo.
6.Hakikisha kama uta amua kutembeza kama kwa wadada, akikisha unakuwa msafi, smat kabis, wadada wengine waoga sana, na pia wanapenda usafi. kuwa msafi. Honyo usichanganye mapenz na biashara. Jitahid utatoka mdogo wangu ila la mwisho fanya hayo yote uku ukimtanguliza Mungu kwanza sala na maombi.
Felix jamani unatoa michango mizuri sana, mimi unanibariki sana natamani nikujue. Kuna mtu aliniamia eti wewe ni kijana mdogo sana na una kamwili kadogo ni kweli?