Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Msafiri Kasian nimenukuu vibaya kaka yangu... Ni Tosha ndio anamvunja moyo ngarambe.
dogo acha ujanja ujanja, tumsaidie au tukusaidie? haya rekebisha upesi ili nirudisaidieni kwa huyu mwenye CHEM -E,BIOS -S NA GEOG -D Atapata chuo na mkopo kweli kwania anapenda asome education....MANY THANKS
mwenye D, S, S nae afanyeje jaman?
Jamani na mimi? Naombeni msaada jamani HIST- S, GEO -E na KISW-D
Mtu ninayemshangaa kabisa ni Tosha, eti anadai kuwa ngarambe hawezi kupata chuo kabisa! Vigezo vilivyowekwa kwa form 6 leavers ni "a minimum of TWO(2) principals".Soma kwenye "Students guidebook 2012/2013" kwenye "preface" pg 7,yenye title "Minimum Entry Requirements into Higher Education Institutions",sasa Tosha,sikuelewi kabisa.
Kwanza asante sana kwa kunisahihisha maana nilikuwa nachukulia experince ya miaka kadha an sikuwa na nia ya kumkatisha tamaa mtu yeyote,infact nimeona mwaka huu minimum qualification kweli ni two principal passes, pili Ngarambe nimepita The Admissions Students Guide Book ya TCU na kubaini baadhi ya vyuo ambavyo minimum institutional Admision points kwa baadhi ya vyuo ni kweli zinaanza 2.0 kwa hiyo unakidhi vigezo katika vyuo vifuatavyo:
1. Bachelor of Education(Arts) na Bachelor of Arts with Education kwa vyuo vilivyoko chini ya Tumaini University kama vile IUCO,TUDARCO,SMMUCo,JoKUCo na center za hivyo vyuo vikuu vishiriki vya tumanini University
2. Bachelor of Arts with Education kwa St. John's University of Tanzania na center zake
3. Bachelor of Education kwa University of Arusha na center zake za Mbeya na Buhare
4. Bachelor of Arts with Education(English,Geo and CTS) na Bachelor of Arts with Education(Engl,Kiswa and CTS) kwa Bagamoyo University
Kuhusu Bachelor of Education in Arts ya Dar es salaam University College and Mkwawa Unviersity College najua kwamba hivi ni vyuo vikuu vishiriki vya UDSM kwahiyo institutional Admission Points zinabaki kuwa 5 points from any 3 subjects licha ya ukweli kwamba DUCE inaonekana imeandikwa 2 from any 3 subject nadhani ni makosa ya kiuandishi kwakuwa mwisho wa siku all academic matters katika vyuo hivi kuanzia muongozo wa udahili,ufundishaji,matokeo ya mitihani mpaka utoaji wa degree ni chini ya Senate ya UDSM so LAZIMA kufafana katika vigezo vya udahili na mambo mengine ya kimsingi ya kitaaluma kwa kuwa degree itakayotolewa ni ya UDSM na siyo DUCE wala MUCE,anyaway unaweza kuulizia kutoka DUCE ili kupata uhakika.
Ngarambe nakutakia mchakato wenye mafanikio.