We kasome sheria! Jitahidi ufaulu vizuri chuoni, mambo hayatakuwa magumu sana kwenye ajira. Hata hivyo ni vyema ujichunguze we binafsi na ujiamulie kwamba unataka kuwa nani. Swala la kutaka kusoma kitu bila kuwa na mapenzi nacho itakuja kuleta hali ya kutokuwa mtaalamu mzuri. Hata hivyo una ndoto nzuri. Binafsi nawashangaa hawa watu wanaokukejeli kwa kutofahamu maana faculty, wakati wao wenyewe wamezaliwa wakiwa hawajui na sasa wanafahamu. Muda ukifika utafahamu mambo kwa upana, si ajabu wengine walikuwa wanadhani chuoni unasoma kombi, heri yako unaelewa japo kidogo.