Ushauri juu ya faculty gani ya kusoma (kuchukua) chuo kikuu

Ushauri juu ya faculty gani ya kusoma (kuchukua) chuo kikuu

HUWEZI KUSOMA FACULTY..! Hamna kitu kinachomewa kinachoitwa Faculty dunia nzima!
 
Hivi unawajua NECTA vizur au unawasikia tu?subiri matokeo kwanza ndo upange hayo mambo yako
 
Mdogo wangu Finder boy kwanza hongera kwa confidence uliyonayo juu ya matokeo tarajiwa lakini uache dirisha kidogo la maumivu kama matokeo hayatakuwa kama upangavyo! Mimi naungana na waliokushauri kama matokeo yakija kama utakavyo kasomee sheria nasisitiza kasome! Vyuo vikuu shahada (degree) sinasomwa (kama ni kiswahili kizuri) na wala hazichukuliwi! nadhani hii dhana ya kusema unachukua shahada fulani inachangia kwa kiasi kufeli kwa wadogo zetu vyuo vikuu! Kasome mdogo wangu!

Asante kaka kwa ushauri.
 
We kasome sheria! Jitahidi ufaulu vizuri chuoni, mambo hayatakuwa magumu sana kwenye ajira. Hata hivyo ni vyema ujichunguze we binafsi na ujiamulie kwamba unataka kuwa nani. Swala la kutaka kusoma kitu bila kuwa na mapenzi nacho itakuja kuleta hali ya kutokuwa mtaalamu mzuri. Hata hivyo una ndoto nzuri. Binafsi nawashangaa hawa watu wanaokukejeli kwa kutofahamu maana faculty, wakati wao wenyewe wamezaliwa wakiwa hawajui na sasa wanafahamu. Muda ukifika utafahamu mambo kwa upana, si ajabu wengine walikuwa wanadhani chuoni unasoma kombi, heri yako unaelewa japo kidogo.

Asante kwa ushauri wako na maneno yako ya busara.
 
Back
Top Bottom