Ushauri juu ya faculty gani ya kusoma (kuchukua) chuo kikuu

Ushauri juu ya faculty gani ya kusoma (kuchukua) chuo kikuu

Polital science ni nzuri tena inatoa, si unacheki wanasiasa wanavyo ila dunia
 
Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita 2013. Nimesoma HKL na ninategemea kupata B ya history, B ya kiswahili, na B ya language. Hivyo naomba ushauri wa faculty gani nzuri ya kusoma chuo ambayo haitanisumbua kupata ajira nikigraduate ( faculty iyo iwe tofauti na Education). Asanteni!
MUNGU AWABARIKI!

Hivi nyie watoto mnataka kulipeleka wapi Taifa letu unataka kusomea Faculty ili uwe nani...sasa nisikilize kwa makini ni kwamba Faculty haisomewi chuo kikuu wanasomea kozi fulani Faculty ni utawala wa kozi mbalimbali.
 
Asante kwa kunielewesha.
 
Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita 2013. Nimesoma HKL na ninategemea kupata B ya history, B ya kiswahili, na B ya language. Hivyo naomba ushauri wa faculty gani nzuri ya kusoma chuo ambayo haitanisumbua kupata ajira nikigraduate ( faculty iyo iwe tofauti na Education). Asanteni!
MUNGU AWABARIKI!

Kijana unakera sio siri..hata kama ni ndoto bac hayo ni maluweluwe, kuomba ushauli ni facult gani usome kama ulisoma hkl si dhambi, lakn unafkia hatua ya kupanga matokeo wakati hujui hata mtihan utakujaje? Baba ako ndo katunga? We unadhan B zinakuja kiholela namna hiyo? Embu subir matokeo kwanza alafu ndo uje na hoja zako hizo ili tukushauli kulingana na uwezo wako.
 
Unataka kusomea faculty? Somo la department unategemea kupataje?? Wewe kiboko!
 
Unataka kusomea faculty? Somo la department unategemea kupataje?? Wewe kiboko!

Ni kitu cha kueleweshana Tongs, sio kuleta kejeli! Nawasiwasi na uwezo wako wakufikiri.
 
Huyu dogo kituko

Nashukuru. Ila wewe kituko zaidi. Umeshindwa kunielewesha unasema kituko! Kama hujui kitu bora ukafunika kombe sio kucomment tu kila unachofikiria. FIKIRI KABLA YA KUTENDA!
 
We kasome sheria! Jitahidi ufaulu vizuri chuoni, mambo hayatakuwa magumu sana kwenye ajira. Hata hivyo ni vyema ujichunguze we binafsi na ujiamulie kwamba unataka kuwa nani. Swala la kutaka kusoma kitu bila kuwa na mapenzi nacho itakuja kuleta hali ya kutokuwa mtaalamu mzuri. Hata hivyo una ndoto nzuri. Binafsi nawashangaa hawa watu wanaokukejeli kwa kutofahamu maana faculty, wakati wao wenyewe wamezaliwa wakiwa hawajui na sasa wanafahamu. Muda ukifika utafahamu mambo kwa upana, si ajabu wengine walikuwa wanadhani chuoni unasoma kombi, heri yako unaelewa japo kidogo.
 
Mdogo wangu Finder boy kwanza hongera kwa confidence uliyonayo juu ya matokeo tarajiwa lakini uache dirisha kidogo la maumivu kama matokeo hayatakuwa kama upangavyo! Mimi naungana na waliokushauri kama matokeo yakija kama utakavyo kasomee sheria nasisitiza kasome! Vyuo vikuu shahada (degree) sinasomwa (kama ni kiswahili kizuri) na wala hazichukuliwi! nadhani hii dhana ya kusema unachukua shahada fulani inachangia kwa kiasi kufeli kwa wadogo zetu vyuo vikuu! Kasome mdogo wangu!
 
Back
Top Bottom