Ushauri juu ya kilimo cha kisasa

Godwin Mmari

Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
30
Reaction score
5
WanaJF,

Kutokana na hali halisi ya biashara nchini Tanzania kuwa tete, nimefikiria na kuamua kuwekeza kwenye sekta ya Kilimo cha Nafaka na Mafuta.

Tayari nimepata sehemu za kuanzia kama Kilosa na Ifakara. Nimelazimika kujiunga nanyi hapa kuomba msaada wa ushauri na changamoto za kilimo kwa sasa.

Nimeona mabandiko mengi kule kwenye Ujasiriamali lakini hayako updated ili nijue pa kuanzia. Awali nilikuwa msomaji tu.

Ahsanteni.
 
Mkuu, taja zao husika unalotaka kudeal nalo ili tuweze kukusaidia namna ya kukabiliana na changamoto zake. Maana ukisema kilimo cha zao litoalo mafuta yapo mengi sana kuanzia maboga,mti wa msalaka, miwese, mbono, mgude, mkorosho n.k
 
Soko la mazao ndiyo kikwazo kikubwa wanachokabiliana nacho wakulima, serikali inahimiza sana wananchi walime kwa bidii, mavuno yakiwa mengi serikali kama kawaida huwakimbia wakulima.
 
Wakuu,
mm1, Ahsante na Kisima
Ahsanteni sana.
Ktk mazao ya nafaka nalenga Mahindi na Mtama ( nina uhakika wa soko la nje) pia mazao ya mafuta ni Alizeti na Karanga.
 
Last edited by a moderator:
Changamoto kubwa ni mabadiliko ya hali ya hewa kama utakuwa unategemea mvua pekee,
ila ukiingia katika mfumo wa irrigation,
basing on dripping irrigation inamafaniki makubwa kwa wakulima,
usiogope kulihudumia shamba nalo litakuhudumia.
 
Wakuu,
mm1, Ahsante na Kisima
Ahsanteni sana.
Ktk mazao ya nafaka nalenga Mahindi na Mtama ( nina uhakika wa soko la nje) pia mazao ya mafuta ni Alizeti na Karanga.

OK Mkuu! Inaonesha unataka kufanya kilimo ktk large scale.
Changamoto ya kwanza kabisa ni kupata eneo kubwa lililo sehemu moja. Uwe makini sana matapeli hata vijijini wapo, haijarishi ni kiongozi au m/kiti wa kijiji/kitongoji. Fuata taratibu husika, ushahidi wa maandishi na video ni mhimu.
Changamoto nyingine ni kupata nguvukazi itakayoendana na kasi yako. Kingine ni uhakika wa kuvuna i mean maji ya uhakika kwa mazao yanayohitaji maji mengi. Jingine ni uhakika wa soko na simamia mwenyewe kazi zako ili usijutie kujihusisha na kilimo.
Ila la kheri KILIMO KINALIPA!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, taja zao husika unalotaka kudeal nalo ili tuweze kukusaidia namna ya kukabiliana na changamoto zake. Maana ukisema kilimo cha zao litoalo mafuta yapo mengi sana kuanzia maboga,mti wa msalaka, miwese, mbono, mgude, mkorosho n.k

Mti wa msalaka na mgude ndo mimea gani hiyo mkuu?!.Naomba unifahamishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…