Ushauri Juu ya kuanza Biashara kwa mtaji wa laki moja

Laki ni ndogo lakini inaweza kukufanya ufike mahali yaani ukuze mtaji kama ifuatavyo..

Chukua 20,000 shona barakoa 150-200 nenda masokoni,kwenye taasisi au wape vijana wakauze kwa shilingi 500 moja.
wapitishie bodaboda,daladala(abiria na madereva) tena kwenye daladala fanya kama wale wajasiriamali wa sabuni uwe muongeaji na uwaelimishe kisha wauzie barakoa ila usipotoshe kuhusu huu ugonjwa. Jikite kuwaeleza faida ya bidhaa yao.

80,000 tafuta mabinti wawili nunua chupa za chai koroga uji wakauze vijiwe mbalimbali asubuhi sana na jioni kwasababu njombe kuna baridi.

Au

Pesa yote kanunue kuku vijiji kwa 7,000 hadi 10,000 kawauzie wenye majiko bar au hotelini ila usiwe na tamaa upate faida kubwa zitakudodea ila ukifocus kwenye kutengeneza wateja wa uhakika hatakama faida ndogo mzigo utakuwa unauza mara kwa mara tena watakusumbua.

vile vile ukiweza ongeza thamani kuku zako sio uwachinje no uza kuku wape wateja ofa ya pilipili au malimao.

e.t.t
 
Mkuu hili ni wazo zuri sana Ngoja nilitafakari kwa kina zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Duh! ..mabarakoa yalivyo mengi hivyo mkuu?
 
wabongo acheze nau kwenye bei na ushawishi...
barakoa 2 kwa 500 kikubwa apige hesabu apate faida ila tatizo letu ni faida kubwa basi hatuzingatii ubora na usalama na mambo mengine..

NB:Sehemu zingine barakoa za vitenge wanauza 1000-2000
Hili ni wazo zuri Ila barakoa naona kama mtu akinunua awezi kununua pia huku zipo nyingi kama naona vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…