nampendayeye
Senior Member
- Mar 24, 2015
- 125
- 71
Ni maziwa gani mazuri ya mtoto wa umri wa miezi miwili. Kwa maana wife anataka kumwanzishia mtoto maziwa kwani likizo ya uzazi ndo inaisha. Naomba msaada wenu wazazi wenye uzoefu na maziwa ya mtoto.
1. Lactogen 1 made from France.
2.NAN 1 made from Holland.
3.S26 made from Republic of Ireland.
4.Infacare 1 from South Africa.
5. SMA 1 from Republic of Ireland.
namba 1,2,3 na 4 hayo yamethibitishwa na TFDA kutumiwa na mama kwa ajili ya mtoto na nje yana maelekezo yake kwa lugha ya kiswahili, namba 5 TFDA wameyakataza kutumiwa na reason kuwa hayan lugha ya kiswahili nje ya kopo kwa ajili ya matumizi ila bado yapo na yanaingia nchini na watu wanayatumia na ni mazur tu.
Asante sana mpendwa. Mungu akubariki sana tena sana. Kwa hiyo rank ilivyo ndo ubora ulivyo? Au hayana tofauti?
Ni maziwa gani mazuri ya mtoto wa umri wa miezi miwili. Kwa maana wife anataka kumwanzishia mtoto maziwa kwani likizo ya uzazi ndo inaisha. Naomba msaada wenu wazazi wenye uzoefu na maziwa ya mtoto.
Hahaaaaa yani wanamukatili mtoto wakijifanya digitalBaba utakuwa umemaliza maziwa ya mtoto
Kwanin asimnyonyeshe miez 6 jaman mkamjengea immunity ya kutosha na hata kama anaenda kazin si akamue tena rahis kweli muhimu mama ale vizr tu haya maziwa ya kopo hasa lactogen sio mazur kabisa na mengi feki labda s26 ndo mazur na yenyewe ni expensive hata kama mnauwezo maziwa ya mama ni muhimu jaman
Hahaaaaa yani wanamukatili mtoto wakijifanya digital
Mtoto anatakiwa kunyonya maziwa ya mama six month sasa haya ya makopo mhhhhhh anunue breast pap awe ana mhifadhiwa anapewa mana wenye watoto hufanya kazi half day
Niwazi kabisa kuwa baba anawivu sana..ameamumua kuja na mkakati kabambe wa kujipa asilimia 100 ya umiliki wa maziwa ya Cowberry
mtu kaomba ushauri wa aina ya maziwa anapewa namna ya kumnyonyesha..
nadhani wengi si wazazi na kama ni wazazi basi hawana situation zinazopelekea mtoto kupewa maziwa mengine,
si rahisi kumnyonyesha mtoto miezi sita kama inavyosemekana labda kama mtu ataamua kuacha kazi na kushinda nyumbani.
Hata breast pump ni nzur badala ya maziwa ya kopo, inshort mtoto anatakiwa anywe maziwa ya mama tu katika ukuwaji wake from newborn to toddler, ila inatokea shida watoto wengne wananyonya mpaka mama akimaliza kumnyonyesha mtoto anakuwa kachoka, wamama wengne maziwa yao mepesi yaan mtoto haongezeki kilo kinakuwa kiduchu, na watoto wengne hawashibi hao, so haya maziwa ya kopo unaweza kumuongezea ili aendelee kwa ukuaji mzur na hayana shida jaman
Breast pump hafu anaya hifadhi vizuri wakati mama hayupo mtoto anatumia. Kama maziwa ya mama mepesi afuate taratibu za vyakula vinaongeza nutrients kama vyakula walavo kina mama walio na pre mature mtoto ataongezeka. Hayo ma lactogen kujidaganya tu. Mtoto anayenyonya vizuri haugui hadi mwaka mzima toka kuzaliwa.
Hili nalo ni tatizo ulaji mubovu una wa cost wengi hasa ulaji wa kimazoea ambao kamwe haumuongezei mtoto uzito. Life lilizo tight mtu anabeba tu matokeo yake sasausemayo kweli dada yangu, nimekuwa muuzaji wa hayo maziwa kwa kipindi tu, tatizo lipo kwa hawa dada zetu wanaopewa mimba vichochoroni na uwezo hawana, wanashindia asubuh vitumbua viwili, chai, ugali kwa kachumbari so inakuwa hatari kwa mtoto kwani kwenye maziwa hapati kitu zaid ya maji mepesi.