Mkuu Riwa asante sana kwa maelezo makini, binafsi niko mbali na dada yangu umenipa kitu kipya khs manjano, ukweli ni kuwa anawashwa sana, ngozi yake imekuwa nyeusi sana na kukakamaa, pia macho yamekuwa njano, naambiwa pia anachoka sana,kutapika,na kuharisha kidogo.
Mkuu amepima vipimo vingi kikiwemo cha ini ameambiwa liko na vipimo vya mara ya mwisho amefanyia kcmc ambapo ataenda tena kesho kwa vipimo vingine nadhani ni hiyo bleda unayosema imeziba, Swali lingine ni kuwa eti kuna operation ya kutumia mionzi bila kupasuliwa? Na manjano inasababishwa pia na nyongo? Je baada ya operation hiyo haitamsumbua tena?
Asante sana nasubiri majibu mkuu