Ushauri juu ya tatizo la nyongo

Ushauri juu ya tatizo la nyongo

Dr Justice

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
797
Reaction score
855
Heshima mbele Wakuu, nina dada yangu ameugua muda mrefu kdg na hosp wamekuwa wakimwambia ni tatizo la nyongo imezidi mwilini na kuzagaa kny damu!

Kwa hakika ametumia dawa nyingi na tumeshawaona specialist wengi lkn bado hali yake inazidi kuwa mbaya! Naombeni wataalamu hapa wanisaidie kujua nyongo ikisambaa kny damu dalili zake ni zipi na inasababishwa na nini?! Nawiwa kujua hilo kwa kuwa imetupa utata sana hivyo natamani nipate maoni ya wakuu hapa,vile vile naomba kujua kama hili tatizo huwa linahitaji operation.

Asanteni
 
Kuna tofauti kidogo kati ya 'nyongo' na 'manjano', japo magonjwa mengi (kama siyo yote) ya nyongo dalili yake ni manjano. Tofauti ni kuwa manjano ya nyongo huwa yanaambatana na kuwashwa mwili. Kama una uhakika tatizo ni nyongo, basi kuna ulazima wa huyo mgonjwa kuonwa na daktari bingwa wa upasuaji, kwa sababu mara nyingi manjano ya nyongo huwa yanasababishwa na kuziba kwa mfuko wa nyongo (gall bladder), na mara nyingi tena kuziba kwa mfuko wa nyongo kunahitaji upasuaji kama tiba.

Kama si nyongo, bado dada atahitaji vipimo mbali mbali hasa vya damu kugundua manjano yake yanasababishwa na nini. Kuna matatizo kadhaa ya damu ambayo husababisha manjano. Manjano pia yanaweza sababishwa na matatizo ya maini, hivyo atahitaji pia kufanya vipimo vya kuonyesha kama ini lake linafanya kazi vyema.

Mpeleke dada kwenye hospitali yenye wataalam na uwezo wa kufanya vipimo hivyo ili tatizo lijulikana na apate tiba inayostahili.
 
Mkuu Riwa asante sana kwa maelezo makini, binafsi niko mbali na dada yangu umenipa kitu kipya khs manjano, ukweli ni kuwa anawashwa sana, ngozi yake imekuwa nyeusi sana na kukakamaa, pia macho yamekuwa njano, naambiwa pia anachoka sana,kutapika,na kuharisha kidogo.

Mkuu amepima vipimo vingi kikiwemo cha ini ameambiwa liko na vipimo vya mara ya mwisho amefanyia kcmc ambapo ataenda tena kesho kwa vipimo vingine nadhani ni hiyo bleda unayosema imeziba, Swali lingine ni kuwa eti kuna operation ya kutumia mionzi bila kupasuliwa? Na manjano inasababishwa pia na nyongo? Je baada ya operation hiyo haitamsumbua tena?

Asante sana nasubiri majibu mkuu
 
Back
Top Bottom