KIXI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2015
- 1,955
- 2,465
Mimi ni kijana nikiishi Mkoa X, ambapo nilikuwa na mchumba ambaye tulibahatika kupata mtoto. Sote tulikuwa na ajira , lakini maisha yakaelekea tofauti, na hatimaye tukakutana na changamoto ambazo zilitupelekea kuachana.
Baada ya kuachana, mchumba wangu alielezea haja ya kuishi kwangu kwa muda ili kujiweka sawa . Nilimruhusu aishi nyumbani kwangu kwa muda wa mwezi mmoja, ingawa wakati huo nilikuwa nimehamishwa kikazi na nipo katika Mkoa mwingine.Nilikuwa nikirudi hom siku moja moja Katika kipindi hicho, kulikuwa na msichana wa kazi ambaye alikuwa akifanya kazi nyumbani kwangu na alikuwa anamlea vizuri mtoto wetu.
Kwa bahati mbaya, wakati nilipokuwa nikienda nyumbani, nikajikuta nikiingia kwenye uhusiano wa kiapenzi na msichana wa kazi kwa siri. Aliweza kunipatia faraja na tukajenga uhusiano mzuri.
Wakati huu, Wazazi wangu walijua kuhusu hali yangu na wamenitaka nirudi kijijini, ambapo tayari ameshapata mchumba mwingine nimuoe. Niliongea na huyu mchumba wa kijijini, na naye ni msichana mzuri na mwenye sifa nzuri,na mpaka sasa nipo naye kwenye mahusiano kwa mwezi mmoja ingawa sijawahi muona physically kutokana na ubize wa kazi , huwa tuwasiliana kwenye simu na kuonana live kupitia watsapp call lakini bado nipo kwenye uhusiano wa siri na msichana wa kazi. Kitu ambacho kilinishangaza Mama mtoto wangu ambaye tumeachana anasema bora nimuoe huyo msichana wa kazi coz anaamini mtoto wake atakuwa kwenye mikono salama
Ninafanya maamuzi magumu kuhusu ni nani ni bora kumuoa kati ya hawa wawili: msichana wa kazi, au yule wa kijijini kwetu.
Ningependa kupata ushauri wa dhati kutoka kwenu.