USHAURI: Kama umeteuliwa na Rais Samia au popote fanya haya. Utanishukuru na hautaishi tena kwa kuhami cheo

USHAURI: Kama umeteuliwa na Rais Samia au popote fanya haya. Utanishukuru na hautaishi tena kwa kuhami cheo

Ukitaka udumu katika nafasi zozote za Uteuzi fanya haya Utanishukuru

1. Acha kufikiri Wewe ni bora kuliko wote waliochwa au unaowaongoza Kumbuka hata wewe Ulikuwa chini ya mtu in before na hicho cheo umeazimwa tu tena ni kwa muda mfupi

2. Acha kudharau watu utakaowakuta huko kwani ni hao ndio waliosababisha yule aondoke na wewe upewe hiyo nafasi yako leo

3. Acha kutegemea kazi Kama chanzo chako kikuu cha mapato ya familia yako kumbuka hakuna Mfanyakazi Tajiri, Ukiutafuta utajiri kazini lazima "Utaiba" na huo ndio utakuwa mwanzo wa Mwisho wako hivyo fungua biashara itakusaidia kukuongezea Kujiamini

3. Usiwadharau watu wa chini yako kwani wananamba ya boss wako watakuchongea kuwa unakiburi & dharau tambua hata mtangulizi wako Ilikuwa hivyo then akatemwa

4. Onesha matokeo chanya muda wote yaani ondoa woga kwenye kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa bila kuathiri wajuu yako

5. Jitahidi ufungue akaunti kwenye mtandao wowote wa kijamii na tumia Ukurasa wako kuelezea mafanikio ya Serikali na Rais aliyekuteua

6. Kuwa Mchamungu ndipo Mungu atakupandisha juu ya hapo

7. Epuka ligi zisizo za lazima na wengine kwakuwa watu wengi wanakawaida ya kutokukubali kushindwa hata kama hawana nguvu kiasi gani lazima wapambane kulipiza kisasi

8. Epuka kujionesha unanguvu zozote zile mfano pesa, wanawake|wanaume, mamlaka kwani utaanzisha vita na wanaodhani ni wao walistahili hizo nguvu|sifa

9. Usitumie cheo chako kuwaliza wengine hata kama ni kwa mademu zao au Ujinga wao kamwe epuka machozi ya binadamu kwani yananguvu ya kisasi

10. Usimsahau aliyesogeza jina lako na CV yako kwa Rais kumbuka CV zako hazina miguu lazima zilipelekwa na Mtu,

11. Tumia hekima zaidi kuliko sheria katika kuongoza

12. Elewa Wewe sio wa kwanza kwenye hicho kiti na hautakuwa wa mwisho hivyo ishi Kama kesho hautakuwepo hapo


#Kabla ya yote toeni Sadaka kushukuru,


[Someni hii na muifanyie kazi mtakuja kunishukuru sana kwenye mikeka ijayo]
Hapo namba 10,utamjuaje mtu aliyepeleka CV Yako kwa Mama?
 
Back
Top Bottom