Ushauri: Kamaliza chuo kaja na mtoto si wangu

Ushauri: Kamaliza chuo kaja na mtoto si wangu

davie dee

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Posts
934
Reaction score
1,213
Habari zenu wana MMU!

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna jamaa yangu hapa yupo kwenye mahusiano na mpenzi wake yapata miaka 6 hivi.

Sasa jamaa alipanga na mpenzi wake kwamba binti akimaliza chuo moja kwa moja afikie alipopanga msela asirudi kwao ili waendeleze mahusiano yao wakiwa kwa msela kwani wazazi wao walikua wanafahamu, basi msela kajipanga ghetto ili demu wake akija aje akute fresh lakini cha kushangaza siku dem anakuja kaja na mtoto mdogo wa miezi tisa.

Alf anamwambia msela alibeba mimba kwa bahati mbaya akaogopa dhambi ya kutoa.

Jamaa yupo njia panda haamini.....
Mbaya zaidi kuna ada alilipa wakati binti yupo chuo na pesa ndogo ndogo alkua akimtumia.

Kaja kuniomba ushauri amtimue dem au maana kampa siku tatu asimkute maana kamsusia hadi ghetto msela karudi kulala kwao.

Binti nae anadai baba mwenye mtoto kamkataa.

Kuna kipindi dem hakurudi kwao akiisingizia anasubiri amalize kabisa maana alkua kabakiza mwaka wa mwisho na ndo kipindi kumbe alkua analea mimba

Mi nimemshauri amtimue tu maana kesho hakawii kuleta mengine.
 
jamaa ni mpole mno ndo maana binti katumia advantage hiyo msela analia kama mtoto yaani
Upole sio shida vishawishi ni vingi na binadamu tumeumbiwa tamaa miaka6 na ukute hawakua karibu kivile kuchapiana nje ipo hio


Vp kama jamaa yako ndo angekua na mtt huyo mdada akakuomba ushauri ungemshauri nn?!
 
Unajitangaza vipi una mchumba tena mnajulikana mpaka makwenu then msionane mara kwa mara?

Yani mpaka mchumba anabeba mimba miezi 9, anazaa, anakuja kwako mtoto ana karibia mwaka hujajua tuu?

Huyu jamaa bado mtoto, mwambie asioe kwa sasa ndoa itamshinda.
 
Poleni yake kona ilikuwa kali wakati ana-over take[emoji848][emoji848]
 
Wewe na jamaa yako wote mnaulemavu...
Na sijui hapa mnataka tuwashauri nini hasa, ilhali tayari binti na mwanae mshaanza kuwatunza...
Minashauri tu mumtafute na mzazi mwenzie na huyo unae muita dem, kisha mumpishe hapo ghetto ili waendelee kuishi pamoja ili wamkuze mtoto na mtoto akisha kuwa ndipo mkamtolee dem mahari na kisha mfunge ndoa
 
Kuna wanaume ni mambumbumbu,na hili ni la kuomba ushauri kwa watu kweli.
 
Mwambie kitanda hakizai haramu
Aendelee kulea mkojo wa mwanaume mwenzake​
 
Back
Top Bottom