Ushauri kati ya paving blocks au kokoto

Ushauri kati ya paving blocks au kokoto

JMF

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
1,758
Reaction score
2,770
Wakuu salaam kwenu.

Naomba kujuzwa gharama na ubora kati ya paving blocks au kokoto kwenye eneo la biashara lenye mita za mraba 40. Kama ni kokoto ni za aina gani na kama ni paving block ni zipi.

Pia naomba kusikia experience toka kwa wadau wanaotumia kimoja wapi kati ya hizo kwenye maeneo yao. Asanteni.
 
Bora paving blocks kwa sababu ya faida zake kuliko kokoto.
  1. Zitadumu zaidi kuliko kokoto (durability), kokoto zitasogezwa huku na huku kadiri wateja wanavyoingia na kutoka
  2. Wateja wanapenda kutembea juu ya paving blocks zaidi kuliko juu ya kokoto (resilient)
  3. Ni rahisi kusafisha paving blocks kuliko kokoto
  4. Gharama hazitofautiani saana, ya paving blocks itakua juu kidogo ila kwa muda mrefu (in the long run) itakua nafuu zaidi.
Kila la kheri mkuu.
 
Weka pavers mkuu tena kwa eneo la biashara unaeza tumia interlock shape au small rectangular tena za zege kabisa, durability yake ni kubwa kama alivyosema juu apo na hautapata stress kipindi hchi cha mvua. Ni Pm kama utahitaji
 
Back
Top Bottom