Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Siku tutakapokuja kuwa na katiba mpya kazi ya ubunge iwekewe vipengele vya kuifanya kuwa kazi ya heshima kulingana na hadhi yake na umuhimu katika nchi.
Mojawapo ya kipengele muhimu sana ni mgombea ubunge awe mkazi ameishi katika jimbo analogombea kwa kipindi cha kuridhisha(mfano angalau miaka 5 mfululizo) kueleka mwaka wa uchaguzi.
Nchi nyingi duniani makini huwezi kuwa mbunge kama wewe sio mkazi wa kudumu kabisa wa jimbo unalogombea au kutaka kuwa mbunge wake.
Ni aibu kubwa ubunge kuonekana kazi ya oya oya inayoweza kupewa yoyote ilimradi amekuwa maarufu tu bila kujali huo umaarufu wake hata ni wa nini.