The BornAgain
JF-Expert Member
- Jun 23, 2024
- 428
- 582
Kuna wakati inatupasa kuendelea kujifunza na kuhimizana kuhusu USHAURI KITAALAMU. Katika jamii ya Watanzania na duniani kote, kuna watu wamejikita katika weledi na pia wenye vipaji fulani. Wengine wana elimu ndogo, za kati, na za juu. Ni wachache wasio na elimu rasmi, ila wana ujuzi na uzoefu kutokana na mazingira wanayotafutia riziki, nk.
Suala la USHAURI wa kitaalamu kuhusu jambo lolote ni muhimu sana katika dunia ya uhangaikaji. Mtindo wa kupata ushauri wa kawaida ambao si rasmi na si wa kitaalamu umekuwa ukitumika sana kwa kuwa unaepusha gharama kadhaa. Ila mdogo mdogo, ushauri wa maeneo kama afya, sheria, mahesabu/uhasibu, nk, unachukua kasi. Ndiyo maana firms nyingi zinafunguliwa. Nadhani watu tumeona kuwa wakati mwingine shortcut ni wrong cut, au rahisi ni gharama!
Ndiyo, ushauri usio rasmi si mbaya, hasa wa marafiki, ndugu, na jamaa, japokuwa si wote watakupa "passwords" za mafanikio yao, hasa njia za mkato walizotumia kufikia mahali walipo. Ndiyo maana hupaswi kuiga haraka. Ila ushauri rasmi unakuwa mzuri zaidi kwa sababu mtoa ushauri naye anataka matokeo. Achana na wale wa "bora ushauri"—hapana! Ushauri wenye commitment ya kufikia yale yaliyoshauriwa ndio bora zaidi.
Mfano, kama ni suala la kibiashara, mmejadili na kuona kuwa mradi au biashara husika inaweza kufanyika kwa sababu ya viashiria chanya vingi vya kupata faida kuliko hasara kwa muda mzuri. Basi wazo la kuandika business plan au proposal linaweza kufanyika, na wewe uliyetoa kazi unafuatilia ushauri huo ili kupata matokeo tarajiwa. Ni kama ushauri wa kiafya; ikiwa daktari atasema unywe dawa mara 3 kwa siku kwa wiki nzima, unywe maji mengi, na kula chakula cha kutosha. Usipofanya hivyo, unaweza kupona nusu nusu na kujiona uko sawa, ila siku chache zijazo ukaumwa tena au kupata tatizo kubwa zaidi. Vivyo hivyo katika mikakati yetu ya kimaendeleo, tunakwama kwa njia hiyo.
MIMI KAMA MSHAURI WA MIRADI, kujadili wazo ni suala muhimu kabla ya kujua tufanye nini kiutekelezaji. Kuna mawazo yanayotakiwa huduma ya upembuzi yakinifu kabla hujaandika andiko lolote. Ni muhimu sana.
Kwa leo, hayo tu.