Ushauri: Katika strategy ya kiuchumi na kielimu, Tanzania itoe Scholarships za kwenda china, hasa kwa waalimu wa VETA, na vyuo vya kati

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Sio siri, wenzetu hawa set up ya elimu yao imejibu tatizo la ajira. Ni kawaida kuwasikia wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda China wanakwambia kwamba nenda na sampo tu, mengine mchina anamaliza. Hawa elimu yao Institute mahitaji ya jamii.

Nashauri waalimu na wanafunzi wa elimu ya kati, kuanzia VETA, Dar es Salaam Institute of Technology, Mbeya kuna chuo kikuu cha sayansi, Vyuo via afya, kilimo, na kadhalika. Kila mwaka itengwe skolaship ya wanafunzi wasiopungua 1000. Waende katika vyuo ambavyo havijajikita katika pure academics. Wake huko, wasome weeee. I am sure after 10 years, tutakuwa mbali.

Hata hao ambao Bashe anawapa mashamba ya mifano, I wish pia wangekuwa wanaandaliwa utaratibu wa training kila mwaka kutoka kwa wataalamu wanaofanya kazi hizo.

Ni aibu mpaka leo hata bajaj inatushinda.
 
Kupeleka watu katika level ya chuo kikuu hakutaleta mabadiliko yoyote yenye tija.
Tunahitaji kufumua mfumo wa elimu kuanzia ngazi ya msingi,syllabus zetu zimejaa ujinga mtupu ,kukariri vitu visivyo na tija katika maisha ya ulimwengu wa sasa.
 
Hawataleta chochote zaidi ya watoto shombe nshombe na mama zao wa kichina . Usifikiri serikali hazifanyi hivyo. Tangu Nyerere mpaka leo vijana wanaenda nchi mbali mbali lakini hakuna Jipya. Kipindi cha kikwete walipokuwa wanaenda kwenye uchimbaji gas walipeleka vijana China na nchi zingine sasa hao watu wameleta impact gani ?
Tuna tapa tapa tu.
 
Sekta ya gesi ni ya kuajiriwa zaidi
 
kwamba kulikuwa hamna mkakati mzuri wa kuwapeleka uko mpaka yanatufika aya na hamna hatua zimechukuliwa zidi Yao?

kama ni ivyo nchi Iko na matatizo hii inabidi kila kitu kifumuliwe kianze upya
 
kwamba kulikuwa hamna mkakati mzuri wa kuwapeleka uko mpaka yanatufika aya na hamna hatua zimechukuliwa zidi Yao?

kama ni ivyo nchi Iko na matatizo hii inabidi kila kitu kifumuliwe kianze upya
Kama nguo imetatuka uzi mmoja tu, unataka ichanwe yote ishonwe upya hata sehemu ambazo ziko vizuri?
 
Kama nguo imetatuka uzi mmoja tu, unataka ichanwe yote ishonwe upya hata sehemu ambazo ziko vizuri?
nguo ninayoizungumzia mimi kwa mtazamo wangu ni haijatatuka, ni imekosewa toka mwanzo,

hata izo sehemu zinaonekana ziko vizuri ni janja janja tu za kuziba ziba baadhi ya maeneo ili nguo ionekane Ilipatiwa toka mwanzo
 
Kwa hiyo unataka hata masomo ya kusoma, kuandika na kuhesabu yafutwe katika shule za msingi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…