Tatizo tumekuwa na kazi ambazo zinahitaji uwezo wa kusimamia miradi na budget mbali mbali za maendeleo. Lakini tunaweka makada ambao wengi wamezoea kupiga domo kucha kutwa bila kufahamu chochote kuhusu uongozi. Hii imesababisha nchi zima na kila idara kuwa ya machawa na watu wasio jielewa jielewa wakati vijana wengi wasomi wenye ujuzi kushinda wanatafuta kazi. Kuna mpaka CPAs wengi na vijana kutoka vyuo vya uongozi hawana kazi na machawa ndiyo wakurugenzi. Yaani ni aibu mpka mkurugenzi anateuliwa na Raisi wakati kuna makatibu wakuu ! Kama ni katiba imepitwa na wakati ibadilishwe.