Ushauri: Kichanga wangu analia sana usiku

Ushauri: Kichanga wangu analia sana usiku

Ni kawaida mkuu mpka afikishe miez mitatu,tumbo huwa linajaa gesi kwa likijaa sana lazima alie kuna dawa flan inaitwa spasmo ni ya maji inauzwa elfu tano huku kwetu nyasincha akilia unamuwekea vitone vitatu mdomoni gesi yote inaisha kabisa na analala vizuri ukienda pharmacy watakupatia maelezo mazuri sana hiyo dawa nzuri sana mkuu.
 
Kwanza unaishi wapi..kama ni dar basi huyo mtto hutakiwi kumvisha nguo nyingi usiku kikubwa kinacho mliza mtto itakuwa ni joto unatakiwa kujua unavyo sikia wewe kwenye hali ya hewa na mtto hujisikia hivyo sio wewe unasikia joto lakini mtoto unamgubika nguo nyingi ...kingine je anapata maziwa ya kutosha?
Nipo mkoani, swala la maziwa namshukuru Mungu napata maziwa ya kutosha,
 
Nakushauri yafuatayo.
Angalia mahusiano yako na mzazi au mmeo. Angalia uhalisia wa mtoto huyo baba yake halisi ni yupi. Washirikishe wazazi upande wa huyo mtoto hata kama wako mbali kuna maneno wakisema yaweza kuwa tiba. Si uchawi ni tamaduni tu. Ni ushauri siyo sheria ikufunge.
Nilijua tu watu kama nyie mtachangia
 
Nakushauri yafuatayo.
Angalia mahusiano yako na mzazi au mmeo. Angalia uhalisia wa mtoto huyo baba yake halisi ni yupi. Washirikishe wazazi upande wa huyo mtoto hata kama wako mbali kuna maneno wakisema yaweza kuwa tiba. Si uchawi ni tamaduni tu. Ni ushauri siyo sheria ikufunge.
Duh!
 
Jibu hili nikma ulikuwa unalisubiria au Mkuu we kiboko
Jamaa ana dharau sana. Anajiona kama matatizo ya watoto anayajua yote. Kuna matatizo ya watoto ambayo hata dokta bingwa hawezi ila yanaisha kitamaduni tu. Sasa atuachie sisi tuliozaa watoto kwenye mafungu kama Yakobo ndo tunaelewa tiba zake na sababisho.
 
Kabisa Mkuu na ulichokiuliza ni cha Msingi kabisa Mtoto kulia kuna mengi kabisa.. Mengi ni ya Kitamaduni na ndiyo maana watu wanapaka majivu au mkaa kwenye paji la uso
 
Ampeleke hospital..aachane na mambo ya imani
Hadi anaingia humu hakujua kama hizo hospital zipo upenuni mwa nyumba yake. Au unadhani sisi hospital huwa hatuendi kutibiwa?. Amekusikia ataenda ila mpaka sasa ukweli kaupata.
 
Nakushauri yafuatayo.
Angalia mahusiano yako na mzazi au mmeo. Angalia uhalisia wa mtoto huyo baba yake halisi ni yupi. Washirikishe wazazi upande wa huyo mtoto hata kama wako mbali kuna maneno wakisema yaweza kuwa tiba. Si uchawi ni tamaduni tu. Ni ushauri siyo sheria ikufunge.
Umenena ukweli
 
Watoto usku huwa wanaona mengi mkuu , vitu vya kutisha hasa ... wakati wa kulala uwe unampakaa wanja katika nyuso zake " mi wa kwangu pia alikuwa hivo lakini nilvokuwa nampaka wanja hakuwa anasumbua tena ..
Kama wa kiume je!
 
Kama ni mtoto wa kiume na sehemu unayoishi ina baridi basi itakuwa ni ngiri inamuumiza mtoto yaani tumbo linamuuma kwa chini ya kitovu, dawa yake ni chukua mizizi ya mitula(ndula) inayootaga porini chemsha maji yake mpe anywe yakiwa ya uvuguvugu tatizo litaisha na usiku mfunike mtoto vizuri na nguo ili baridi isimpate
 
Nina binti angu sasa ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu kanatembea sasa

Nakumbuka hakuna kipindi nilichoteseka kama baba ndani pindi ana umri wa miezi mitatu,alikuwa analia balaa usiku mamake nilikuwa namwonea huruma maana halali

Ikabidi niende hospitali lakini wakaniambia hapo hana tatizo ni stage tu ya ukuuaji

Ikabidi nibadili ratiba,saa kumi na moja jioni nalala nikitoka job,saa mbili usiku naamka naanza kufanya kazi za kiofisi huku namsubiri aanzishe timbwili nianze kumbembeleza

Tabia hii ipo mpka sasa kwa umri huu wake,lakini si kama kipindi kile
Hongera sana baba.

Mie alikiuwa akilia nafanganya naumwa maana aio kazi rahisi.. First born alikuwa analia hadi na Mimi nalia, 2nd hajasimbua kwakweli.
 
Back
Top Bottom