Ushauri: Kichanga wangu analia sana usiku

Ushauri: Kichanga wangu analia sana usiku

Mwanangu anaumri wa miezi miwili, kipindi cha nyuma mambo yalikua shwari hakua na tabia ya kulia usiku hivi karibuni tabia yake imebadilika na usiku wa kuamkia leo ndo imekua funga kazi, mtoto ameanza kulia gafla kilio kikali kilichojaa uchungu ndani yake kwa sauti ya juu sana.

Kitu kilichofanya mwili wake upoe na awe akitoka jasho kila sehemu ya mwili wake kama amemwagiwa maji, ilikua ni hali inayoongopesha sana maana tulibembeleza na kuembeleza baada ya mda mrefu alinyamaza kwa kupitiwa usingizi mwili wake ukiwa umechoka sana.

Hana ugojwa wala haumwi popote maana mda wa mchana anakua mchangamfu na mwenye afya tele ila usiku hulia kwa kiasi cha juu sana naombeni ushauri kwa yeyote aliyewahi kukutana na hali hii ama mwenye kujua nini kifanyike kukomesha hali hii.
Natanguliza shukurani.
Hakikisheni wazazi wote wawili mnaoga vizuri kwa sabuni nzur zenye kuondoa jasho la mwili, vinyweleo makwapani mtoe maana harufu yake huenda ikawa inamdhuru mtoto jengeni utaratibu wa kupiga mswaki kila mnapotaka kulala, hakikisheni mtoto mnamuweka mbali kidogo na ninyi ili kumuepusha na audible lambling zenu(ushuzi) kama tatizo litakuwa bado endelevu mkamuone Dr. Haraka sana.
 
Ndio njia pekee mtoto anaweza kuwasiliana na wanaomlea aweze kupata msaada ndivyo anavyowasilisha woga wake, maumivu yake ya tumbo ( Mara nyingi kutokana na kujaa gesi) , njaa , kulowana kwa mavazi yake n.k.

Mnyonyeshe vya kutosha ( ideally kila baada ya Massa 2), ukiwa na mtoto wa umri huo usilale gizani ili anaamka mwanga uwepo ( ingawa hawaoni uzuri mbali but mwanga ukiwapo woga hupungua),

Ukihisi ni maumivu ya tumbo kujaa gesi weka tumbo began au mchezeshe miguu juu chini na kumminya vidole vya miguu taratibu, pia waweza kutumia maji special yaka kupunguza gasi kulingana na Dr atakavyokushsuri na upatikanaji wake.

Kulia usiku kwa mtoto wa umri huu inafikirika kuwa ni survival mechanism anaifanya unconsciously but ni njia mojawapo ya kudelay kuzaliwa mtoto mwingine, ikumbukwe mtoto mwingine akizaliwa mapema care yake na lishe vinakuwa mashakani.

Kwa Julia na kumsumbua mama usiku , mama anakuwa stressed, ovulation very unlikely kutokea kwa hiyo mimba za haraka/ chapchap zinahairishwa. Hata mgegedo pia sio rahisi nyakati za stress.

Kwa msaada zaidi na uelewa mpana, Fanya matumizi sahihi ya smart phone yako - google " why news babies cry at night" , utapata maarifa ya kutosha ya kukusaidia wewe na wengine ili kuepukana na swaga za anaona vibwengo au anataka jina la babu.
Jpili njema.
Umesema yote chief, Bravo [emoji122][emoji122][emoji122]

Nimependa ulivyomaliza kabisa kabisa wengi wangeanza kufikiri witchcraft manyuva [emoji23][emoji28][emoji23]
 
Watoto usiku huwa wanaona mengi mkuu , vitu vya kutisha hasa wakati wa kulala uwe unampakaa wanja katika nyuso zake " mi wa kwangu pia alikuwa hivo lakini nilvokuwa nampaka wanja hakuwa anasumbua tena .
[emoji15] [emoji15] [emoji15] kwq jinsia zote ?
 
Kawaone wabibi wa mambo ya watoto wachanga watakusiadia
 
Nakushauri yafuatayo.
Angalia mahusiano yako na mzazi au mmeo angalia uhalisia wa mtoto huyo baba yake halisi ni yupi washirikishe wazazi upande wa huyo mtoto hata kama wako mbali kuna maneno wakisema yaweza kuwa tiba si uchawi ni tamaduni tu ni ushauri siyo sheria ikufunge.
uko sawa hata mimi wa kwangu alikuwa analia lakini wazee waliposema neno moja tu akawa analala mpaka anaamushwa
 
A) Mtoto wangu wakiume alitusumbua sana usiku hatukuwa tunalala kwa kulia tulibadilishana, sasa amekuwa ya darasa la nne.

Siku moja kwa kuchoshwa nikampa maji ya yaliyopowa akiwa mchanga wa mwezi mmoja yalikuwa ya chai nikapoza yakabaki na uvuguvugu kidogo

Nikamuwekea mdomoni aliyafakamia kichizi na baada ya hapo akalala mpaka asubuhi nikajuwa njaaa muda wote nikimpa vimaji wife amelala kwa uchovu wakubembeleza tulikuwa tunapeana zamu

Ilipofika asubuhi nikaenda kununua maziwa special ya watoto Aspen one.kwa wachanga chini ya miezi 6 na Aspen two kwa walio zaid nikamsimulia wife yaliyotokea usiku.

Ikawa tunayaandaa maziwa na ile chupa ya kunyonya akianza kulia anapewa maziwa ananyonyaaa akishiba basi analala mpaka asubuhi

Nb: chupa yakumnyonyeshea mtoto kila siku ichemshe kwenye maji ya moto kabisa kama ya chai kuuwa vijidudu...chupa na vifaa vyake vyote.mifuniko nk.....otherwise atapata magonjwa ndani ya muda mfupi kama kuharisha au kuumwa tumbo, nk

B) Hakikisha mtoto halali na nguo mbichi zenye mkojo mkojo huwasha sana kila wakati mkaguwe awe mkavu

C) Hakikisha unampeleka hospitali kuthibitisha kweli yuko salama na hana matatizo mengine.

D) Usithubutu kulala na mwanao mchanga ukiwa umetoka kufanya mapenzi nje ya mkeo kwa wanaume hakika mtoto atawasumbuwa sana, ukifanya uchepukaji usimshike mtoto wala kulala kwenye eneo lake kaa mbali kabisa na kichanga

Kwa wanawake vilevile jitahidi kulea mtoto mpaka akuwe, ukiwa nakichanga, mpe baba halisi tu hiyo mashine sio vinginevo ukigawa kwa baba asiye wa kichanga hakika utauguza nakutaabika sana

Sielewi kwanini hii D) ni suala la itikadi na imani lakini nikweli it works 100% ukitaka uepuke mateso ya kuuguza mtoto nakukesha usiku usipuuze kwa wababa ukichepuka jitenge na mama na kichanga oga vilivyo

Kwa leo ni hayo tu ndimi mzazi mwaminifu Adolay
miezi 6 ya kwanza mtoto haitakiwi apewe chochote zaid ya ziwa la mama.
 
Watoto usiku huwa wanaona mengi mkuu , vitu vya kutisha hasa wakati wa kulala uwe unampakaa wanja katika nyuso zake " mi wa kwangu pia alikuwa hivo lakini nilvokuwa nampaka wanja hakuwa anasumbua tena .
Mmh!
 
Hongera sana baba.

Mie alikiuwa akilia nafanganya naumwa maana aio kazi rahisi.. First born alikuwa analia hadi na Mimi nalia, 2nd hajasimbua kwakweli.
Shukrani kwa pongezi

Kama ulivyosema kulea ni kazi kuliko kuzaa,kwa hili nawaheshimu sana wanawake waliokuza wanawe ,wengne hata bila wenzi wao
 
Hakikisheni wazazi wote wawili mnaoga vizuri kwa sabuni nzur zenye kuondoa jasho la mwili, vinyweleo makwapani mtoe maana harufu yake huenda ikawa inamdhuru mtoto jengeni utaratibu wa kupiga mswaki kila mnapotaka kulala, hakikisheni mtoto mnamuweka mbali kidogo na ninyi ili kumuepusha na audible lambling zenu(ushuzi) kama tatizo litakuwa bado endelevu mkamuone Dr. Haraka sana.
Duh! Jamani kazi kweli kweli
 
I had the same issue,
sasa hivi mwanangu ana miezi mitatu na siku 16 .mwezi wa pili ulikuwa changamoto tulikuwa tunapokezana kumbeleza . ni normal case kama mchangiaji mmoja hapo juu alivyoeleza. nunca de creer itakwisha cha msingi mama asiache kumnyonyesha na na nguo za kumvalisha usiku ziangalieni san zisije kuwa ni nzito sana au nyepesi sana kwani ni rahisi kusababisha pneumonia kwa mtoto joto husababisha pneumonia(high humidity)
 
Nina binti angu sasa ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu kanatembea sasa

Nakumbuka hakuna kipindi nilichoteseka kama baba ndani pindi ana umri wa miezi mitatu,alikuwa analia balaa usiku mamake nilikuwa namwonea huruma maana halali

Ikabidi niende hospitali lakini wakaniambia hapo hana tatizo ni stage tu ya ukuuaji

Ikabidi nibadili ratiba,saa kumi na moja jioni nalala nikitoka job,saa mbili usiku naamka naanza kufanya kazi za kiofisi huku namsubiri aanzishe timbwili nianze kumbembeleza

Tabia hii ipo mpka sasa kwa umri huu wake,lakini si kama kipindi kile
Pole sana hii imenikuta tokea mtoto wangu akiwa na wiki mbili alikua analia na hivi ana sauti kubwa yani hadi majirani wanaamka wanadhani huwenda kuna tatizo limetukuta ndani, tunabembeleza usiku kucha na inapofika alfajiri analala na mchana wote analala, hivyo mchana wake ukawa usiku kwa miezi 7 mfululizo hakika tuliona rangi zote, analala mmoja unabembeleza ukichoka unampa mwenzako anapambana wewe unalala.

Ukienda hospital hana tatizo na ana afya njema kabisa na alianza kula akiwa na wezi mmoja tu.

Kwasasa ana miaka 4 na miezi kadhaa japo tabia yake ya kudeka bado anayo napambana nae.

Malezi sio mchezo.
 
Jamaa ana dharau sana. Anajiona kama matatizo ya watoto anayajua yote. Kuna matatizo ya watoto ambayo hata dokta bingwa hawezi ila yanaisha kitamaduni tu. Sasa atuachie sisi tuliozaa watoto kwenye mafungu kama Yakobo ndo tunaelewa tiba zake na sababisho.
Hii ilinikuta kwenye fungu moja japo sitaweka wazi yote, ila imani za kitamaduni hakika zipo, mtoto alimtesa sana mama yake, nilipofika na kumshika sikio tokea siku hiyo ikawa tiba hadi leo yupo shule
 
Pole sana hii imenikuta tokea mtoto wangu akiwa na wiki mbili alikua analia na hivi ana sauti kubwa yani hadi majirani wanaamka wanadhani huwenda kuna tatizo limetukuta ndani, tunabembeleza usiku kucha na inapofika alfajiri analala na mchana wote analala, hivyo mchana wake ukawa usiku kwa miezi 7 mfululizo hakika tuliona rangi zote, analala mmoja unabembeleza ukichoka unampa mwenzako anapambana wewe unalala.

Ukienda hospital hana tatizo na ana afya njema kabisa na alianza kula akiwa na wezi mmoja tu.

Kwasasa ana miaka 4 na miezi kadhaa japo tabia yake ya kudeka bado anayo napambana nae.

Malezi sio mchezo.
Kula mwezi mmoja? Mlikuwa mnamrisha chakula gani mkuu?? Maana kitaalamu mtoto chini ya miezi 6 inashauriwa anyonyeshwe maziwa ya mama tu,bila maji wala kitu chochote.

Mkuu pengine mwanao anaponyosha hashibi,au maziwa ya mama ni mepesi. Ale Mchele,mihogo,nazi vitu kama hivo vitasaidia katika upande wa maziwa ya mama.
Lakini pia kama mpo dar tazameni hali ya hewa hii,joto nyuzi 34 mkimvalisha nguo mingi kero kwake,kama mnalala na feni pia tatizo. Kama mpo kwenye baridi mkamvalisha nguo kiduchu akapigwa na baridi pia tatizo.
Wababa,msikimbilie kuwapa watoto wenu maji ya kunywa au maziwa ya kopo au vyakula when they are under 6 months kwa ushauri wa kitabibu.
 
Kama analia kwa kushtuka na sauti kali na ana mwili sana uwe unaponda kitunguu swaum unakifunga kwenye kitambaa unaweka jiran na kichwani akilala,... Mimi wangu pia ana miezi miwili wiki ilopita yote hatujalala ilikua timbwili hadi tulipoambiwa tufanye hivyo kwmb ni dalili ya degedege na huwakumba sana watoto wanene
 
Pole sana hii imenikuta tokea mtoto wangu akiwa na wiki mbili alikua analia na hivi ana sauti kubwa yani hadi majirani wanaamka wanadhani huwenda kuna tatizo limetukuta ndani, tunabembeleza usiku kucha na inapofika alfajiri analala na mchana wote analala, hivyo mchana wake ukawa usiku kwa miezi 7 mfululizo hakika tuliona rangi zote, analala mmoja unabembeleza ukichoka unampa mwenzako anapambana wewe unalala.

Ukienda hospital hana tatizo na ana afya njema kabisa na alianza kula akiwa na wezi mmoja tu.

Kwasasa ana miaka 4 na miezi kadhaa japo tabia yake ya kudeka bado anayo napambana nae.

Malezi sio mchezo.
Mkuu

Congratulations being dady to yr family,unaonesha unawajibika vyema kabisa
 
Back
Top Bottom