Ushauri!!Kichwa kunguruma kama ingine ya gari

Daffi Jr

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Posts
3,824
Reaction score
909
Habari za humu mabibi na mwabwana!!Ni muda mrefu nina tatizo la kichwa!!Nikikaa sehemu tulivu isiyo na kelele kuna hali isiyokuwa ya kawaida naisikia kichwani mwangu!!'Kelele za magari' !Kichwa kinanguruma kama mlio wa gari kubwa!Hakiumi wala sisikii hali yetote iliyotofauti!!Nakereka na hii hali maana muda wote ni kama magari yanapishana kichwani mwangu!!!Kwa kuwa humu kuna wataalamu wa kila aina naombeni msaada wenu!Nini sababu na tiba yake!!Nisaidieni wapendwa
 
unaugonjwa fulani ambao sijui ni upi ulio anza kuwa sugu cha msingi go for medical checkup ukifanikiwa kuudhibiti hali yako itarudi kama awali.
 
Mkuu kazania dini na mambo ya sala sana
...sio dalili nzuri kiroho..tafuta mchungaji wa kipentekoste atakuelewesha zaidi
Wewe ndiyo hovyo kabisa, badala umwambie amtafute YESU eti tafuta mchungaji wa kipentekoste shida yenu, mnawatafuta sana watumishi wa Mungu zaidi ya mnavyomtafuta Yesu.

Ugua moyoni mwako Mungu hayuko kwa mchunhaji au kwa kanisa fulani yupo rohoni mwako, huwa naumia sana mtu unapoamini sana katika kuombewa bila wewe mwenyewe kujitafakari, YESU hajawahi tibu mtu katika muujiza wake kwa nguvu zake mwenyewe mara zote alisema IMANI YAKO IMEKUPONYA why watu mnaamini sana kuombewa kabla ya toba, kufunga na kuomba na kubadirika kuacha dhambi?????
 
Hiyo kitu sijawahi jaribu mkuu
Pole sana nenda hospital usikae, chukua hatua afya ni muhimu saaaana. Ukichelewa watakuja kusema Wamekukamata umeficha magari yao kichwani mwako, hawana dogo hawa!!
 
Vip Mkuu Historia Yako Kuanzia Ulipozaliwa Mazingira Uliyokulia Na Mahali Unapoishi Unaweza Kueleza Kwa Ufupi Tukusaidie
 
Kakikatie bima kubwa vinginevyo itakula kwako.
 
hospital wakishindwa nenda kwa sangom mkuu
 
Yesu alipaa kwenda Mbingun zaid ya 2000 years ago. Sasa unaposema amtafute mm unanchanganya
 
Jombaa hujawahi kupiga cha arusha kweli?
 
Huo ni ugonjwa ndugu yangu, mm mwenyewe nliugua ila kwa sasa unakuja na kutoka. Ugonjwa unaitwa tinitus. Unasikia sauti kikoloni wanaitwa buzzing sound. Na husababishwa na either kutumia headphones kwa sauti ya juu kwa mda mrefu, kama shuguli zako ni dj, ama unafanya kazi kiwandani nankuna kelele nyingi. Inasababishwa na kukaa mda mrefu katika kelele hivyo ngoma ya masikio huathirika na hutuma taarifa kwenye neuron huko ndani kabisa katikati ndo sauti hutokea. Tiba, jiepushe na na kutumia headphone, kusikiliza mziki sauti za juu. Au huwa kuna aina ya miziki ukiwa kazini, ukilala usiku uvae headphone na ufungulie kwa sauti ya chini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…