Ushauri: Kila shule ya sekondari pawepo na angalau mwalimu 1 wa somo la Ufundi stadi

Ushauri: Kila shule ya sekondari pawepo na angalau mwalimu 1 wa somo la Ufundi stadi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Huu ni ushauri wangu wa mwisho kwa serikali.

Yaani namaanisha hapa nimetumia akili zangu zote kuwaza namna ya kuondoa ujinga na umaskini katika jamii.
Sasa % kubwa ya watoto wa darasa la saba wanajiunga kidato cha kwanza.

Wengi huishika kidato cha 4 kwasababu mbalimbali.

Miaka 4 ya sekondari imekuwa kama sehemu ya makuzi tu kwasasa.

Na wengine huendelea na elimu ya kati mpaka juu lakini bado changamoto ni zilezile.

Sasa ni wakati muafaka wa elimu ya sekondari kuifanya ELIMU MSETO.

Angalau mtu akimaliza kidato cha 4 anaweza kwenda workshop na kuomba kusaidia kazi au kuajiriwa kama fundi msaidizi.

Kwa wenye idea ya ujasiriamali wanaweza kujiajiri.

Ni utumwa mkubwa kama taifa kufundishana ujasiriamali wa kuuziana bidhaa za kichina.

Tukidanya ujasiriamali wa kuuziana bidhaa za kichina hapo tunaijenga Uchina na si Tanzania, lakini vijana wakitumia ufundi kubuni na kuunda vitu vyao tutalijenga taifa.

Watu wakipata ujuzi hapo ndipo tuanze kufikiri namna ya kuwakopesha mitaji na vitendea kazi.
 
Back
Top Bottom