Ushauri kuepuka madeni ya taifa

Ushauri kuepuka madeni ya taifa

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Posts
2,252
Reaction score
1,041
Hivi karibuni Ndg. Ludovick Utoh, Mkaguzi naMdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),alisema kuwa hali ya nchiya Tanzania kiuchumi kwa maana ya mapato na matumizi si nzuri na kwamba deni laTaifa limefikia tillioni 25 (billioni elfu 25).Aliyasema hayo akiwa Dodoma kwenye mkutano wa pili wabaraza la wafanyakazi wa ukaguzi nchini.

Ushauri aliotoa: Serikali na Bunge wajitathimini,Serikali isimamie vizuri vyanzo vyake vya mapato na matumizi.

Lengo langu hapa si kujadili

  1. Hali iliyopelekea hatua hii tuliyonayo (deni kufikia Tilllioni 25)
  2. Matumizi yanayo aksi deni hilo kwa maana ya tija au matokeo yanayoonekana au kupimika kulingana na deni hilo

Watanzania wenzangu,
Unajua watu wa hali ya kawaida kama sisi hatuna mahalipa kusemea, kutolea dukuduku letu au hata kuuliza maswali. Wawakilishi wetu naowako bize. Ukipata jukwaa kama hili unashukuru mungu, sasa basi

Kwa vile JF ni chombo muhimu na mtandao mkubwa wakupashana habari za kijamii hapa Tanzania,
Na kwa kuwa Ofisi ya Takwimu ya Taifa jhaijatoataarifa ya matokeo kamili ya sensa ya watu na makazi kwa Umma (nasema hivyo kwasababu sijaona repoti yake kamili ukiachilia mbali baadhi ya taarifa – summary),

Naomba kwa hekima na taadhima kubwa, wachumi wetu,taasisi za kiraia, ofisi ya takwimu ya Taifa, TRA, wizara ya Fedha na wadau wengine, kwa kutumia sensa ya watuna makazi ya mwaka 2012,

  1. Idadi

  • a)Tanzania ina idadi kiasigani cha watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 80 kwa mujibu wa sensa yamwaka 2012?
  • b) Ni idadi kiasi gani chawafanyakazi Tanzania (Wazawa na wageni)
  • c) Wanayo idadi yawafanyabiashara (mmoja mmoja, makampuni binafsi) achilia mbali usahihi wake? Je, ni kiasi gani?
  • d) Wanayo idadi ya wakulimana wafugaji nchi nzima? Je, ni kiasi gani?
2. Ni kiasi gani cha kodi kinachokusanywa kutoka kila kundi b) hadi d)? Kwa mpangilio wa ki-asilimia, ukoje?


3. Ni kiasi gani cha fedha kutoka mapato yatokano ya tozo mbalimbali za huduma zitolewazo na taasisi za Umma? Mfano, Vyuo, Idara za serikali (vibali, service charge, kodi, maliasili, nk). Je fedha yote inayokusanywa ni asilimia ngapi kulinganisha na mapato yanayopatikana kutoka swali namba 2?


4. Kwa vile makato ya kodi ya serikali kutoka kwa mishahara ya watumishi sekta binafsi na watumishi wa Umma inakatwa kwa kila anachopata mfanyakazi, Je mapato ya Mbunge (mshahara na marupurupu mengine yote) ni kiasi gani ? Na je, kwa mwaka, Serikali ya Tanzania inatumia fedha kiasi gani katika kuwalipa (mishahara na malipo mengine) wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ? Na je, ni kodi kiasi gani hukusanywa kutoka katika malipo hayo ? na Je ni asilimia ngapi?


5. Je mapato halisi ya kila mtanzania kutoka kila kundi hapo juu b) hadi d) yanafahamika? Nini mlinganyo wa kiasilimia kimapato kwa kila kundi ukijumlisha na mbunge ? na je, Mlinganyo wao ukoje katika kulipa kodi ?



Kama sikueleweka vizuri na unahitaji ufafanuzi zaidinaweza kufanya hivyo.


Asante sana,

Naomba kuwakilisha kwa ajili ya majibu kutoka kwa wadauhusika.
Josam



 
Usisahau kuwa hiyo serikali yako unayosema inawalisha wanafunzi wa sekondari boarding ambapo wewe unalipia elfu 70 tu kwa mwaka.hata kwa akili ya haraka haraka elfu sabini ni ndogo sana.
Bila kusahau wanafunzi wa chuo wanaopewa mikopo ya elimu ya juu na hawarudishi.
Tatizo la waafrika wanaangalia sana wanasiasa wanajua wao ndio kila kitu,it wrong.
 
Huku ni kutufanya mapimbi tu...Pesa wakope kufadhili shughuli za kiserikali kisha mzigo aje abebeshwe masikini ambaye baada ya kukosa fursa ya kwenda shule aliamua kuwa mjasiriamali kwenye ufugaji na kilimo na bado mazao yake yanapigwa dana dana na wajanja ndo alipe kodi kupunguza deni asilojua lilikopwa kwa matumizi gani? Siku nyingine tutaihoji serikali matumizi ya so called mikopo toka kwa wahisani!
 
Usisahau kuwa hiyo serikali yako unayosema inawalisha wanafunzi wa sekondari boarding ambapo wewe unalipia elfu 70 tu kwa mwaka.hata kwa akili ya haraka haraka elfu sabini ni ndogo sana.
Bila kusahau wanafunzi wa chuo wanaopewa mikopo ya elimu ya juu na hawarudishi.
Tatizo la waafrika wanaangalia sana wanasiasa wanajua wao ndio kila kitu,it wrong.

Sawa huo ni mtazamo tu. Sikutaka kujikita kwenye matumizi, ninachojaribu kufikirisha wadau hapa ni kiasi gani tunakusanya kama kodi kutoka kwa makundi niliyotaja.

Najua kuna vyanzo vingine vingi vya kodi. Hiyo siyo agenda yangu kwa sasa. Lakini haizuiwi kuvitaja na kuainisha mapungufu yake ili yafanyiwe kazi na wasimamizi wa sheria husika. Mfano ni kodi kiasi gani tunakusanya kutoka kwenye wamilii wa nyumba mijini kwa mujibu sheria za Nchi? Na je, kiasi hicho kina aksi uhalisia / idadi kamili ya nyumba zote zilipo mijini au hazijulikani idadi yake? na vyanzo vingine kadha kadha....
 
Back
Top Bottom