ushauri kufanya kilimo

ushauri kufanya kilimo

Kusindika mazao kuna njia nyingi sana kulingana na aina ya zao,kwa hiyo teknolojia nayo ni tofauti. Unapokoboa mahindi na kusaga kupata unga na pumba, tayari umeongeza thamani ya mahindi yako, sijui hapa kama kuna utalaamu sana. Au kukamua alizeti au karanga au kukamua miwa ( wapemba mitaani kwetu na juisi ya miwa) au asali, mbona mashine za kazi hizo zipo nyingi sana mpaka za bei za kutupa kabisa. Mashine ya kusindika asali nimepata kwa jamaa, huenda 2014 nitaanza kusindika mwenyewe asali mbichi.

Wakati fulani nilikwenda Singida, SIDO BLOCK, nikaona vile viwanda pale vya kusindika alizeti, ujenzi na mitambo upo mikononi mwangu. Nilirudi kwetu nikakuta Wakinga wamezifunga mashine kama 12 ktk mji wetu lakini raw materials ni kidogo, kule vijijini umeme haujafika. Nimeamua nijenge ghara kwanza na moto wa REA ukifika nifunge mitambo yangu.

Kazi ipo kusindika matunda, hii kazi ya kusindika nyanya na matunda mengine nimeifanya sana, tatizo ni lile lile la umeme vijijini. Kusindika maziwa kuna tatizo la raw materials.

Mkuu MALILA popote ulipo na wengine.
Nilitaka kujua Gharama za Mashine za kusindika Asali.
Na pia Zinapatikana wapi.
 
Mkuu MALILA popote ulipo na wengine.
Nilitaka kujua Gharama za Mashine za kusindika Asali.
Na pia Zinapatikana wapi.

Nimekusukumia pm, pitia hiyo pm kisha fanyia kazi. Kisha tupe feedback kutujulisha uliyoyakuta huko.
 
Back
Top Bottom