Ushauri kuhusu biashara ya bisi

Englishlady

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
2,736
Reaction score
3,644
Wadau wajasiriamali ninawasalimu!

Naomba kupewa ushauri wa ujasiriamali mdogo bisi.

Huwa napenda sana kula bisi, kila nikipita wanakokaanga lazima ninunue nijilieeee, sasa kwa mapenzi haya nikatamani nami nifanye biashara hii, nimefanya kautafiti kidogo maeneo ya mtaani kwetu hamna wakaanga bisi, nikabaini maeneo kama mawili yanayopitwa na watu sana, nikaona niweke mashine zangu maeneo hayo, nikawauliza vijana wkaanga bisi pale mwenge kuhusu mashine wakanambia zinapatika kwa bei ya laki tatu za kutengenezwa hapa nyumbanina kuhusu mapato ya siku, wakasema huwa wanamaliza mfuko wa kilo20 kwa siku na hupata laki na ishirini mpka na nusu kwa siku. Sasa kabla sijaanza naomba ushauri kwa mwenye uzoefu wa biashara hii, kwani nitaajiri vijana, mie ni mwajiriwa.

Asanteni sana wapendwa.
 
Itakuwa vyema ukiajiri MTU kwakuwa itakusaidia kuwa na vyanzo vya mapato tofauti na wewe kutoacha kazi uliyo ajiriwa..
 
Mi pia huwa naitamani kuifanya,ila napendelea zaidi zile zenye flavor mbali mbali kama tangawizi,kahawa nk.

Mwenye ujuzi na hizo atujuze,hizo mkuu hata ofisini unapeleka.
 
Mi pia huwa naitamani kuifanya,ila napendelea zaidi zile zenye flavor mbali mbali kama tangawizi,kahawa nk.

Mwenye ujuzi na hizo atujuze,hizo mkuu hata ofisini unapeleka.

Hee kukbe kuna ladha mbalimbali sikujuwa hili, ngoja nijifunze.
 
Ishu ni kupata mt ambaye atajal kaz yake msaf na mwamnf at lst hata kwa asilimia 80%
 
https://www.jamiiforums.com//index.php?task=97394
 
Na pia mashine ilizunguka kariakoo hata laki mbli na nusu unapata na garant ya mwaka mzma nimeshafanya research juu ya hlo
 
Mi pia huwa naitamani kuifanya,ila napendelea zaidi zile zenye flavor mbali mbali kama tangawizi,kahawa nk.

Mwenye ujuzi na hizo atujuze,hizo mkuu hata ofisini unapeleka.

mi nilijua ladha ya bisi inatokona na chumv tu, kumbe kuna za design iyo!!!!?
 
Laki na ishirini kwa siku? Are you serious? Kumbe inalipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…