Ushauri kuhusu biashara ya grocery

Ushauri kuhusu biashara ya grocery

Eddy Elphazi

Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
8
Reaction score
9
Habarini za wakati huu wana JF

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu nina miaka takriban mitatu mtaani sjabahatika kupata ajira so nikawa najichanga changa kwenye mambo yangu nikapata kama 2.2 M nikafungua kigrocery mtaani sasa kinachonisibu asee yan nakopwa so mchezo hadi msingi umepungua sana.

Of course nimekaza sana kutokukopesha but kwa wenye uzoefu na hii biashara mnaelewa ni ngumu kiasi gani kumkatalia kila mteja(make wateja wengine ni wateja wako wakubwa) sasa shida inakuja ukimkopa wengine wanakimbia wengine wanalipa ila wanachelewa sana kulipa(hela inabidi izunguke) na msingi unapungua kila kukicha.

Sasa nilikuwa naomba ushauri kwa mwenye uzoefu na hii biashara ni kwa namna gani nitaeza kukabiliana na hili swala la madeni make nataka kabisa niache kukopesha(japo huezi acha kwa 100%).Naombeni ushauri ndugu zangu
 
No bill. It's cash only and money first then service.
 
Habarini za wakati huu wana JF

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu nina miaka takriban mitatu mtaani sjabahatika kupata ajira so nikawa najichanga changa kwenye mambo yangu nikapata kama 2.2 M nikafungua kigrocery mtaani sasa kinachonisibu asee yan nakopwa so
Aisee usipokuwa na roho ngumu utaishia kuvuna mabua.. Hamisha hiyo biashara mahali pasipo na kujuana kwingi.. Binadamu hawana shukrani wala haya wanakukopa ukifilisika ndio wa kwanza kukucheka![emoji35][emoji34]

Nilizika 8M hivi hivi naona.. Mauzo daily si chini ya laki2 lakini cash haifiki 30...
Kingine huko utakapohamia punguza ukaribu na wateja hasa wale wanotaka kukuzoea kwa haraka
 
Hiyo biashara ni ngumu mno. Yaani mpaka uuze chupa 20 ndio upate faida ya elf 5! biashara hii inawafaa wanawake ambapo huifanya kama kichaka cha kujifichia kudanga..
 
Aisee usipokuwa na roho ngumu utaishia kuvuna mabua.. Hamisha hiyo biashara mahali pasipo na kujuana kwingi.. Binadamu hawana shukrani wala haya wanakukopa ukifilisika ndio wa kwanza kukucheka![emoji35][emoji34]
Nilizika 8M hivi hivi naona.. Mauzo daily si chini ya laki2 lakini cash haifiki 30...
Kingine huko utakapohamia punguza ukaribu na wateja hasa wale wanotaka kukuzoea kwa haraka
Asante sana kwa ushauri so mwenyewe ulifanya biashara kama hii?
 
Weka kaunta kauzu...wahudumu ndio walipe madeni...yaani muhudum akikopesha mtu..yeye ndio ahusike kwenye kulipa asidaiwe mteja.
Kuna sehemu niliona muhudumu ndio anahusika na kuna daftari anasaini kaunta kuwa nimechukua vinywaji kiasi kadhaa sijatoa hela..

Aweke kaunta kauzu na hii njia itamsaidia sana
 
Aisee usipokuwa na roho ngumu utaishia kuvuna mabua.. Hamisha hiyo biashara mahali pasipo na kujuana kwingi.. Binadamu hawana shukrani wala haya wanakukopa ukifilisika ndio wa kwanza kukucheka![emoji35][emoji34]

Nilizika 8M hivi hivi naona.. Mauzo daily si chini ya laki2 lakini cash haifiki 30...
Kingine huko utakapohamia punguza ukaribu na wateja hasa wale wanotaka kukuzoea kwa haraka
Hata ulozi haukufanya kazi..😂
 
Hii biashara inamazingira yake!,ukitaka uifanye vizuri lazima uchague mazingira ya kutotegemea wale wateja wa kila siku hawa ndo wakopaji haswa!..
Inatakiwa hata mtu akiingia ye mwenyewe akihitaji kukopa tu anajishuku!.
Nawewe pia upunguze mazoea na wateja,Kama hauwezi ukauzu weka mtu kauzu anaejua kucheka na wateja lakini ajue kwanini acheke nao na kwanini asichekenao!..

Kufanya hii biashara kwenye mazingira local itakuumiza tu maana watanzania wengi vipato vyao haviwaruhusu kunywa kila siku,wakati wanakiu cha pombe kila siku!.
Mazingira ya kukopwa unayatengeneza mwenyewe jua na financial status za wateja wako au eneo ulilopo.
 
Usiweke urafiki kwenye biashara... kama kukopwa kuwe na kikomo...
 
Kopesha kwa unaojua watalipa kwa mda mfupi, wengine zingatia tu "kauli nzuri" . Usikate tamaa, polepole tu uweke ",nidhamu ya pesa" mwisho utatoboa.
 
Inaonekana na wewe huwa unakunywa nao hapo hapo, wanakopa wanazungusha na wewe upo pamoja nao. Ni vigumu sana kuwanyima mkopo kama unafanya hivyo.

Weka kaunta imara asimamie ambaye ndiye utafunga hesabu za mauzo naye.

NB: FUNGA HESABU ZA MAUZO KILA SIKU ASUBUHI KABLA MANUNUZI YOYOTE KUFANYIKA.
 
Back
Top Bottom