Ushauri kuhusu Biashara ya Kuuza Computer: Laptop/dektop used

Ohh! Umeeleza vizuri mkuu! Vipi kuhusu muonekano wa hizo Laptop kwa nje ukoje ? Zinamvutia mteja au zinaonekana used sana?

ndio unachagua mkuu, zinakuepo za kila muonekano.
 
Kama unapesa nenda Dubai. Faida lazima upate, sijui chpchote kuhusu dubai ila kuna watu nawafahamu japo hawawezi kunipa details za huko lakini wanaenda sana kufuata Laptop huko.

Kama huwezi, na unaujuzi wa PC, tafuta kizimba machinga complex fanya mahusiano mazuri na wale jamaa utapata connection zote za kupata hata hizo no test. Ni pesa yako tu. Ila ujue na ufundi kidogo ili uwe unazifufua baadhi.
 
Maelezo mazuri mkuu! Na nimeyapokea!
 
Boss nikija kariakoo duka lako liko sehemu gani,,,, mi nahitaji laptop ya kuniwezesha kuandaa taarifa na mambo madogo madogo,,,, kikubwa isiwe pasua kichwa kwamba ukiitoa kwenye chaji na yenyewe inazima au nusu saa tu inazima,,, na bajeti yangu hata nikipata hizo unazouza 250k,,, kama unaona inafaa utanisaidia zaidi
 
kazi nzur bro nakupataje niachie mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…