RAYAN THE DON
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 679
- 1,218
Habari zenu wanabodi.
Bila kupoteza muda wanabodi. Ni kwamba mwaka 2018 nilifungua duka la vipodozi, nywele bandia za kila aina pale Ubungo.
Nilianza na mtaji wa 2M mbali na hela niliyolipa kodi, kutafuta leseni, n.k. Baada ya kuanza biashara, kila baada ya miezi 2 nilikuwa naongeza 2M ili mtaji ufikie 10M. Katika duka hilo nilimueka mama wa mtoto wangu ili awe ndiye analisimamia hilo duka ili mambo yakienda vizuri liwe linamsaidia yeye na huyo mtoto wetu. Cha kushangaza ni kwamba tangu mwaka 2018 mpaka leo sijawahi kuuza mauzo ya siku moja hata Tzs 50k.
Kila nikijitahidi kuboresha ili nizidi kupata wateja wengi hali ndiyo inazidi kuwa mbaya. Nikienda kupiga mahesabu kwa mwezi unakuta kuna 50k, 20k etc. Nikihoji mauzo yanaendaje majibu ninayopewa ni kwamba biashara imekuwa ngumu wateja hawaji. Nikihoji naomba kuona daftari la mauzo, faida n.k unakuta anasusa na ananuna.
Sasa je dhana ya kwamba duka hujiendesha ni ipi? Kwa sababu hata kodi ya pango ni hela ambayo natoa kwenye vitega uchumi vyangu vingine. Sasa wanabodi kwa mazingira haya kweli nitatoboa? au inachukua muda gani ili biashara ijiendeshe yenyewe? hilo duka limekuwa ni liability kubwa sana kwa upande wangu kwa sababu kodi ya pango ni hela yangu binafsi na wakati mwingine huwa naombwa hela ya kununua mzigo mpya nikimhoji hatoi majibu yanayoeleweka.
Wanabodi nivumilie au niuze duka tu nifanye mambo mengine? kwa sababu nimekuwa nikitoamchango mkubwa sana ila duka halileti faida yoyote.
Karibuni kwa ushauri wenu wanabodi.
Ahsanteni sana.