Ushauri kuhusu biashara yangu

Ushauri kuhusu biashara yangu

RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
679
Reaction score
1,218
Habari zenu wanabodi.

Bila kupoteza muda wanabodi. Ni kwamba mwaka 2018 nilifungua duka la vipodozi, nywele bandia za kila aina pale Ubungo.

Nilianza na mtaji wa 2M mbali na hela niliyolipa kodi, kutafuta leseni, n.k. Baada ya kuanza biashara, kila baada ya miezi 2 nilikuwa naongeza 2M ili mtaji ufikie 10M. Katika duka hilo nilimueka mama wa mtoto wangu ili awe ndiye analisimamia hilo duka ili mambo yakienda vizuri liwe linamsaidia yeye na huyo mtoto wetu. Cha kushangaza ni kwamba tangu mwaka 2018 mpaka leo sijawahi kuuza mauzo ya siku moja hata Tzs 50k.

Kila nikijitahidi kuboresha ili nizidi kupata wateja wengi hali ndiyo inazidi kuwa mbaya. Nikienda kupiga mahesabu kwa mwezi unakuta kuna 50k, 20k etc. Nikihoji mauzo yanaendaje majibu ninayopewa ni kwamba biashara imekuwa ngumu wateja hawaji. Nikihoji naomba kuona daftari la mauzo, faida n.k unakuta anasusa na ananuna.

Sasa je dhana ya kwamba duka hujiendesha ni ipi? Kwa sababu hata kodi ya pango ni hela ambayo natoa kwenye vitega uchumi vyangu vingine. Sasa wanabodi kwa mazingira haya kweli nitatoboa? au inachukua muda gani ili biashara ijiendeshe yenyewe? hilo duka limekuwa ni liability kubwa sana kwa upande wangu kwa sababu kodi ya pango ni hela yangu binafsi na wakati mwingine huwa naombwa hela ya kununua mzigo mpya nikimhoji hatoi majibu yanayoeleweka.

Wanabodi nivumilie au niuze duka tu nifanye mambo mengine? kwa sababu nimekuwa nikitoamchango mkubwa sana ila duka halileti faida yoyote.

Karibuni kwa ushauri wenu wanabodi.

Ahsanteni sana.
 
Pole sana,sasa ww fanya hivi. Kodii ikiisha ya dukani mwambie sina hela. Mzigo ukiisha dukani mwambie sina hela kisha uone nn kitafata Ikiwa tu, labda pesa ya dukani ndio analipa kodi ya anapokaa , kumlipia mtoto ada na mahitaji mengine zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapigwa hapo na huyo mama mtoto wako kwa mujibu wa maelezo yako. Cha kufanya achana na hilo duka, endelea kuwekeza zaidi kwenye mizunguko yako mingine inayokupa pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo bi dada hapo dukani maelewano yako na yeye yako vipi! Ukute anapau nyumba tayari huko Sala sala!
Duka usiuze zaidi ya 50k, hii ni ajabu, duka lenyewe umesema unajichanga lifikie 10mil. Tuseme lina mtaji wa 5mil, halafu mauzo kwa siku hayafiki 50k?

Jaribu kukaa hapo kibandani kwa walau wiki moja uthibitishe. Ikiwa kweli mauzo hayafiki 50k kwa siku, na mtaji ndiyo kama huo 5+mil, hilo duka weka geto uwe unakula kimoja kimoja.
 
Hayafiki kabisa mkuu. Ukizingatia lina mika miwili mpaka sasa hivi mkuu.

Maelewano yako vizuri. Maendeleo ya duka ndiyo yananipa wakati mgumu sana.
 
Pole sana,sasa ww fanya hivi. Kodii ikiisha ya dukani mwambie sina hela. Mzigo ukiisha dukani mwambie sina hela kisha uone nn kitafata Ikiwa tu ,, labda pesa ya dukani ndio analipa kodi ya anapokaa , kumlipia mtoto ada na mahitaji mengine zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Brother kodi ya nyumba ya huyo mwana mama huwa nalipa mimi kwa sababu anaishi na mwanangu. Mwanangu bado ni mdogo sana. Hivyo sitaki ahangaike akamharibu mtoto. Nampenda sana mtoto wangu na sitaki apate taabu and that's why niliamua kufungua hilo duka ili akifika umri wa kwenda shule liwe linasaidia.
 
Ndugu yangu hiyo ishu hata ilipata kunitokea nilifungua duka mwisho kila nikiongeza hela naona inapungua tu sasa kwa sababu mimi ni mzoefu na biashala ya duka nikaona napigwa nikalipa fremu miezi nikaongeza 2mil ya mtaji then nikaliacha ili mwisho lilifilisika tu na nilifanya hivyo baada ya kuona mwanamke duka anafanya kama kitega uchumi chake peke yake wakati mi nilikuwa nazamia mikoani naleta michele kwa kuunga unga tu
 
Mkuu uzembe ni wako:

Ingia dukani fanya stock takin .nini kipo na nini hakipo dukan vilivyopungua ongezea weka kumbukumbu kwenye daftari kisha kila baada ya week let say ijumaa unatenga muda wako unaingia kufanya hesabu ya week nini kimeuzwa nini kimebaki. Ukifanya hivi utapata physical answers kwamba je ni kweli duka haliuzi au linauza hela inapotelea hewani.

Hiki kiliwah nitokea mahali nikatenga muda nikaingia mzigon kufanya uadit za mara kwa mara nikagundua hakukua na wizi ila mbinu za kupata wateja hazikuwepo! Nikatengeneza new stategy ikiwemo kuweka huduma zingine ..kushusha bei na kusaka wateja mitaani kwa mabango. Changes zilionekana.

In short hutak kujishugulisha na hilo duka kwa jasho na maumivu ndio maana huelew nini cha kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Yan ushauri n kuwa n katika maduka yote yanayohusisha mambo ya wanawake weka mwanaume auze. Mwanamke anaweza kmchukia mteja kwakuwa tu kapendeza zaidi yake.

Lakini kwakuw umeamua kuanzisha biashara ili apate walau kujikim, lipa kodi kisha muachie aendelee. Yaani usiingilie chchte. Muache aliendeshe mwenyewe.

Huko kujali, Kujifanya unajua kuulizia hali ya mtoto na biashara ndo kunkokuponza.

Mwanaume inabd uwe na msimamo. Ukishaweka democracy tu kwa mwanamke umekwisha

Ila cha kuongeza mtaftie mtoto bima ya afya. Mama ushamuanzshia biashara. Mengneyo utahusika kwenye kesi ya mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani stock utokaji wake ukoje? Kama bidhaa hazitoki sawa ila kàma zinatoka hapo unapigwa.Ni muda wa kuwa serious arudi nyumbani uajiri mtu ambaye utaweza muwajibisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi niseme hapo mwanamke anapitia mlango wa uwani ..tenga muda wako jaribu upate taarifa pale unapo ingia mzigo mpya record au ata piga picha iwe vizuri kukumbuka. Ikitokea wikiendi umepata muda pita utazame duka na kuangalia vilivyouzwa vina endana na uhalisia

Unajua wanawake ni rahisi kushawishika ukute yuko anacheza michezo yao ya pesa ,au kuna mahali zaidi anapeleka
 
Nimewahi kufanya kazi na mzee mmoja pale Njombe; ana maduka matatu ya spare za magari. Mkataba wa mimi na yeye ulikuwa wa kumfungia system ya kuratibu maduka yote matatu. Pamoja na mambo mengine mfumo ulikuwa na lengo la kudhibiti upotevu wa pesa; maana nahisi mzee alihisi kitu. Now guess what - msimamizi mkuu wa maduka yote alikuwa ni mke wake. Siku ya kwanza nimefika, mzee akamwambia "Kuanzia leo huyu kijana atasimamia zoezi la kufunga hesabu kwa maduka yote!"... sura ya mama ikabadilika mpaka nikaogopa.

Fast forward:
Mama alitumia kila njia nisiendelee kubaki pale na nisifunge mfumo kama tulivyokubaliana. Nilicho-observe ni hiki; Mauzo kwa siku hayapungui TZS Milioni 1 kwa duka moja. Siku ikiwa nzuri yanaenda mpaka Milioni 3. Lakini kila siku lazima mama alikuwa anachukua nusu ya mauzo anaingiza kwenye M-pesa yake. Na mzee anapewa hesabu iliyobaki. Ubaya mzee si mkaaji mara nyingi anakuwa mishemishe kutafuta spare mjini Dsm.

Nikaja kugundua mchezo kwenye invoice pia. Suppliers wakituma mzigo wanaleta na invoice... sasa kwa kila invoice iliyotua pale wakati mimi nipo, kulikuwa na ongezeko la angalau TZS 500,000/=. Nikagundua huo ni mchongo alioutengeneza mama, maana zile invoice mzee huwa hazipitii anaangalia tu TOTAL AMOUNT. Imagine kama huu mchezo umefanyika for years.

Katika kutaka kudadisi zaidi ndipo nikagundua KWANZA huu uhuni anaofanya mama ulisababishwa na mzee mwenyewe. Kwanza nikaambiwa kwa muda mrefu mzee alimtelekeza yule mama. Mzee alikuwa bize na totoz. Sema mama akapambana mpaka mzee akamweka dukani. Kwa hiyo dizaini kama mama anafidia. PILI nikaambiwa mzee ameanza biashara siku nyingi sana lakini hakuwahi kufanya cha maana. TATU nikaja kufahamu kuwa zile hela ambazo yule maza anachomoa daily anazipeleka kwenye ujenzi wa nyumba ambazo hata mzee mwenyewe hajui kama zinajengwa (Ziko 2)!!!! NNE mzee ana gari, lakini nikaambiwa lilinunuliwa na maza kwa staili hiyo hiyo ya kuchomoa pesa na kuziweka kushoto kimya kimya.

Nilipoyafahamu hayo, niliondoka kimya kimyaaaaaa.

BOTTOM LINE.
Inaonesha kuna shida kati yenu wawili - either hakuna TRUST kati yenu wote au yeye ndo sio mwaminifu kiasi ambacho anaamua kufanya mambo yake kimya kimya bila kukushirikisha. Pamoja na juhudi unazofanya kuboresha biashara, usipotatua changamoto inayomfanya asiwe huru kukushirikisha harakati zake - itakuwa kazi bure. Inawezekana kabisa mauzo yakawa ni zaidi ya 50K kwa siku; lakini anazipeleka wapi? Kwanini anafanya hivyo? Je, ana poor money management au kuna kitu anakifanya purposely? Maswali ni mengi, majibu mnayo wewe na yeye tu. Sisi wengine ni sawa na mashabiki uwanjani.
 
Habari zenu wanabodi.

Bila kupoteza muda wanabodi. Ni kwamba mwaka 2018 nilifungua duka la vipodozi, nywele bandia za kila aina pale ubungo.

Nilianza na mtaji wa 2M mbali na hela niliyolipa kodi, kutafuta leseni, n.k. Baada ya kuanza biashara, kila baada ya miezi 2 nilikuwa naongeza 2M ili mtaji ufikie 10M. Katika duka hilo nilimueka mama wa mtoto wangu ili awe ndiye analisimamia hilo duka ili mambo yakienda vizuri liwe linamsaidia yeye na huyo mtoto wetu. Cha kushangaza ni kwamba tangu mwaka 2018 mpaka leo sijawahi kuuza mauzo ya siku moja hata Tzs 50k.

Kila nikijitahidi kuboresha ili nizidi kupata wateja wengi hali ndiyo inazidi kuwa mbaya. Nikienda kupiga mahesabu kwa mwezi unakuta kuna 50k, 20k etc.

Nikihoji mauzo yanaendaje majibu ninayopewa ni kwamba biashara imekuwa ngumu wateja hawaji. Nikihoji naomba kuona daftari la mauzo, faida n.k unakuta anasusa na ananuna.

Sasa je dhana ya kwamba duka hujiendesha ni ipi? kwa sababu hata kodi ya pango ni hela ambayo natoa kwenye vitega uchumi vyangu vingine.

Sasa wanabodi kwa mazingira haya kweli nitatoboa? au inachukua muda gani ili biashara ijiendeshe yenyewe? hilo duka limekuwa ni liability kubwa sana kwa upande wangu kwa sababu kodi ya pango ni hela yangu binafsi na wakati mwingine huwa naombwa hela ya kununua mzigo mpya nikimhoji hatoi majibu yanayoeleweka.

Wanabodi nivumilie au niuze duka tu nifanye mambo mengine? kwa sababu nimekuwa nikitoamchango mkubwa sana ila duka halileti faida yoyote.

Karibuni kwa ushauri wenu wanabodi.
Ahsanteni sana.
Mkeo ni kabila gani! isije ikawa anajenga kwao!
 
Nimependa hapo mwisho umeondoka kimya kimya. Ukawaacha na yao

Back
Top Bottom