Hii kozi ni nzuri sana, lakini kwa TZ ni vigumu sana kupata kazi kwenye Halmashauri za (w) ambazo ndo zinachukua graduate wengi, kiufupi hakuna ngazi yako katika Halmashauri za (w). eg Halmashauri zinachuua waalim, madaktari mabwana mifugo etc. ila kuanzia mwaka jana baadhi ya wizara zimeanza kuwatambua graduate wa mol.Biol& Biotech. eg wizara ya kilimo imewaajiri wengi tuu na kuwapeleka kwenye centers zao Mikocheni (MARI),Mbeya, Mwanza etc. Wizara ya mifugo nayo itawahitaji vijana wanaojua molecular biology hasa baada ya Agency yao(CVL) kuanza kazi rasmi. vilevile kuna graduate wengi wanafanya research na centers za hapa nchini. eg. NIMRI, Ifakara centers, KCMC, na miradi mingi ya utafiti iliyopo Universities eg SUA, UDSM, KCMC,Bugando, Muhimbili, etc Unaweza vilevile kuajiliwa na Private centers like pharmaceutical industry, Breweries company, Environmental care centers, Private universities as a Tutor (universities nyingi zinafundisha intr. to mol. biol&Biotech na hawana waalim). Mwisho unaweza kujiajiri, mpaka sasa nishaona group mbili waliojiajiri tayari, Moja ni graduate wa SUA ambao wamejiunga na graduate wenzao wa medical field na kuanzisha Diagnostic lab DSM. wanapima malaria, TB, HIV,MIMBA, Kisukari. etc. Group ya pili ni graduate wa UDSM ambao wameanzisha kampuni ya kuzoa Biological waste from different industries, Hospitals etc and they properly dispose those waste as per biological safety rules and regulation rqments. Hawa wameingia ubia na hospital kadhaa jijini na wana zoa Syringes, contaminated gloves, Pamba, etc. kiufupi uchafu wote wa hospital. group hili limeajiri graduate wenzao wapatao 50. Kama unasoma kazana ufaulu opportunity zipo nyingi zinakuja kwani hii ni kozi mpya sana nchini. wanaoajiriwa Wizarani Range ya mshahara ni kati ya laki 5-8.5. Private nyingi ni laki 9- million 3.5 inategemea kazi na umuhimu wako hapo kazini, ila ni contract basis na sio permanent.