Ushauri kuhusu BSc. Irrigation and Water Resources Engineering

kindimu

Member
Joined
Mar 26, 2014
Posts
42
Reaction score
7
Wana jamvi, ninamatumaini yangu kuwa ni wazima. Mimi nimemaliza diploma ya computer engineering nikabahatika kupata ila ya mkataba katika kampuni moja lakini pia mwaka jana niliomba chuo nikabahatika kupata SUA.

Kwenye fani ya BSc. Irrigation and Water Resources Engineering pia nikapata mkopo 100% nikaenda kuomba nisome mwaka huu na nikakubaliwa.

Sasa naona muda unakaribia na sijapata maelezo ya kutosha kuhusiana na kozi hiyo katika suala zima la kujiajiri au kuajilwa ili nisije kujuta. Mwenye uelewa na kozi hiyo tafadhari naomba anisadie.
 
achana na hayo makozi utapata bp tu. soma sales and marketing. mimi nimepita hapo 1999 bsc agric eng majanga tu
 
Hiyo ni engineering mkuu.Iko vizuri sana.Kwa watu wa civil walio branch huko wanakula shavu sana

Miradi ya maji ya WB,IMF etc wanasimamia wapo.Pesa iko ndefu
 
Hii nchi inavyoende enda kozi kama hizo zimekuwa kama umeingia chaka vile.
Do your home work, fuatilia job opportunities kwa miezi kama 2 hivi. Afu utaona kama kuna kazi hata 1 inayotaka degree kama yako..
 
Hapana mkuu kozi ina soko sana hii aisee Nina ndugu zangu wameisoma hii
 
achana na hayo makozi utapata bp tu. soma sales and marketing. mimi nimepita hapo 1999 bsc agric eng majanga tu
Embu fafanua hayo majanga ni yapi?
Hii nchi inavyoende enda kozi kama hizo zimekuwa kama umeingia chaka vile.
Do your home work, fuatilia job opportunities kwa miezi kama 2 hivi. Afu utaona kama kuna kazi hata 1 inayotaka degree kama yako..

hapa unamaanisha nini?
 
nenda chuo kasome achana na stress za mtaani hela kitaa ipo?
 
Somea BA "Who I know in Goverment". Ajira moja kwa moja BoT.
 
soma upishi mana hotel zinajengwa nyingi sana,, kama unaangalia ajira
 
Agr. Engineering na Irrigation full ajira. hakuna kutangaza serikalini. pia, BRN kwa kilimo ni kilimo cha umwagiliaji naona soko litaongezeka zaidi miaka ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…