Ushauri kuhusu dalili izi za ugonjwa

Joined
Jan 9, 2013
Posts
26
Reaction score
12
Samahani wadau hasa madocta, mtoto wangu ana dalili hii ya ugonjwa ikifika saa nane usiku anapata homa kali mno na ikifika saa kumi na mbili asubuhi homa huisha na anarudi hali ya kawaida tatizo ni muda wa saa nane hadi saa kumi na mbili ni SIKU YA TATU SASA hali hii inajirudia. Nimempeleka hospitali mara ya kwaza alipima malaria, choo, na UTI hakuwa na magonjwa hayo, jana karudi kupimwa upya hosipitali tofauti jibu likaja choo chafu ila haharishi wala kuumia tumbo na choo ya kawaida. NAOMBENI USHAURI JAMANI WATAALAMU.
 
Polee sana jitahidi umrudishe tena hospitali. Homa ni ishara mwili hauko sawa inawezekana hata ana bacteria kwa damu akapate hata antibiotic.
 
Polee saana jitahidi umrudishe tena hosp homa ni ishara mwili hauko sawa inawezekana hata ana bacteria kwa damu akapate hata antibiotic.
Asante sana kwa ushauri, ninawaza kupima hata typhoid maana nashangaa ukimkuta anacheza mchana utazani hana tatizo
 
Yes fanya hivyo. Mimi huwa inatokea hivyo kwa mtoto wangu pia. Mchana anacheza vizuri ila usiku homa.

Malaria hakuna wala UTI lakini Dkt. akiangalia Full Blood picture huwa anagundua infection kwa damu akipata dawa tuu anarespond haraka.

Kwani umemfanyia kipimo cha full blood picture?
Asante sana kwa ushauri, ninawaza kupima hata typhoid maana nashangaa ukimkuta anacheza mchana utazani hana tatizo
 
Hapana sijamfanyia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…