Culturelessman
Member
- Jan 9, 2013
- 26
- 12
Samahani wadau hasa madocta, mtoto wangu ana dalili hii ya ugonjwa ikifika saa nane usiku anapata homa kali mno na ikifika saa kumi na mbili asubuhi homa huisha na anarudi hali ya kawaida tatizo ni muda wa saa nane hadi saa kumi na mbili ni SIKU YA TATU SASA hali hii inajirudia. Nimempeleka hospitali mara ya kwaza alipima malaria, choo, na UTI hakuwa na magonjwa hayo, jana karudi kupimwa upya hosipitali tofauti jibu likaja choo chafu ila haharishi wala kuumia tumbo na choo ya kawaida. NAOMBENI USHAURI JAMANI WATAALAMU.