Binafsi kwa uzoefu wangu kutumia gx 110 (miaka 2)
Route za mjini inatembea kati ya km 7 - mpaka 8km kwa litre 1.
Kwa masafa marefu nimegundua vitu viwili kutoka kwenye hii gari
1. Ukitembea speed chini 100 hasa 80, fuel consumption yake inapungua.
2. Ukitembea speed zaid ya 100 inakula mafuta sana, ni gari yenye mtindo wa kutegemea ukanyagaji wa wafuta; jinsi unavyokanyaga mafuta fuel consumption inaongezeka.
Huu ndio uzoefu wangu halisi juu ya hii gari..
Uzuri wake ni gari comfortable, barabarani imetulia hasa masafa marefu.