Ushauri kuhusu Kilimo cha Tikiti Sugar Queen F1

Ushauri kuhusu Kilimo cha Tikiti Sugar Queen F1

Joined
Jun 13, 2024
Posts
8
Reaction score
7
Habari za Asubuhi wadaunwa sekta ya Kilimo,

Naomba kuuliza je ni siku ngapi mbegu ya tikiti ya sugar queen F1 toka hutumia hadi kutoka ardhini maana ya kwangu ni siku ya tisa bado haijatoka na nimeanzà kupata mashaka ushauri wàdau 🙏
 
Hivi kwanini mnaandika upuuzi kama huu? Kama haujui kitu si unakaa kimya tu mpumbavu wewe?
Mimi ni mpumbavu ni kweli kwa sababu nimeshindwa kujua hata mbegu za matikiti zinaota baada ya muda gani! Lakini najishughulisha na kilimo cha matikiti!
 
Mimi nakushauri tu ongeza bidii katika kazi yako usikwazike na wasiopenda maendeleo yako.
 
Mimi nakushauri tu ongeza bidii katika kazi yako usikwazike na wasiopenda maendeleo yako.
Mkuu pita hapa kidogo

Unapohitaji kupanda tikiti hakikisha umeziloweka kwenye maji masaa12 ama zaidi Kisha zitoe zifunge kwenye kitambaa Cha cotton na uzimwagie maji.

Baada ya hapo ziache Tena masaa12 kesho yake panda zitakuwa zimeanza kupasuka (kuashiria kuota)

Ukipanda hesabu siku3 tu zote zimeota vzr

ZINGATIA:Usiweke udongo mwingi pindi unapopanda. Ahsantee
 
Shimo lake liwe na urefu fani, na umbali wa shimo na shimo ni kiasi gani?
 
Shimo lake liwe na urefu fani, na umbali wa shimo na shimo ni kiasi gani?
Binafisi Mimi hupanda mita1 shina Hadi shina na mstari Hadi msatari ni mit1:30-50 Hivi

Urefu wa shimo(nadhani ulimanisha kina?) hapo Sina kipimo sahihi maana Huwa natifua tifua sana naweza kisia ni sm25-30 hiv kulingana na ardhi yenyewe.
 
Habari za Asubuhi wadaunwa sekta ya Kilimo,

Naomba kuuliza je ni siku ngapi mbegu ya tikiti ya sugar queen F1 toka hutumia hadi kutoka ardhini maana ya kwangu ni siku ya tisa bado haijatoka na nimeanzà kupata mashaka ushauri wàdau 🙏
Tunaomba msitulishe sumu hizi
 
Attachments

  • VID-20250310-WA0020.mp4
    17.5 MB
sm 30 ni sawa na futi moja kwenda chini. Hiyo mbegu itaota kweli?
Hujaelewa ila vile umeuliza naomba nikujibu .....

Cm30 ni kina cha shimo kwenda chini sio kina cha kupanda yaani unatifua kusaidia mizizi kupenya kwa urahisi kwenda chini zaidi. Ni sawa na unapopanda zabibu wanachimbo hadi kiunoni wanavyosema wao kisha kuweka mbolea kwa matabaka kama 2-3 lengo ni hilohilo kuifanya mizizi ipate chakula na kupenya kwa urahisi.

Niliwahi kwenda semina moja tukafundishwa nyanya inatakiwa uchimbe kina futi moja na nusu na futi [cm30] iwekewe majani makavu ya nafaka au miti. Kisha weka udongo.

Mdogo sana kisha mbolea ilichanganywa na mchanga kisha panda nyanya yako.

Lengo ni kwamba ndani ya mwezi zile nyasi kule chini zitaoza na kuwa mbolea pia zitakuwa zinahifadhi unyevyu wa kutosha.

Nyanya zilizaa sana mkuu kwenye shina moja nilikuwa nahesabu hadi 211 matunda hayo! Na nililima mashing 517 tu watu walisomba mno.

Hata sasa huaa napanda mashing kama matano5 kaa ajiri ya matumizi ya nyumbani japo huwa sipigi sumu wala mbolea za viwandani lkani huwa nahesabu matunda hayapungui 80!
 
Back
Top Bottom