ufumawicha
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 504
- 209
Ndugu wanajf wiki moja iliyopita nilikuja hapa na kuwashukuru kuwa baada ya kunishauri kuwa nifungue genge kwa kamtaji kangu kale ka sh.350,000/=.Nimefanikiwa kufungua genge kwa sh.100000/=na iliyobaki nimeweka kaduka kadogo nyuma ya genge.Nilienda TRA wanikadirie kodi kwa miezi 6 kwani nina mpango wa kuwa wakala wa MPESA,TIGO PESA ikibidi na AIRTEL MONEY.TRA waliniambia kwa miezi sita nitalipia sh.318,000/=ili nipewe tin number na kuanza kuitumia nilipe kwa pamoja nusu ya kodi hiyo,sh.159,000/=Kwa kuwa mauzo ni mazuri kwani kwa siku nauza kati ya sh.23000 na sh.35000 kwangu hiyo ni pesa kubwa kwani ndo naanza na niko kati ya watu wenye mitaji mikubwa mithili ya mlima kilimanjaro.Nimejipigapiga na jana nimelipia hiyo nusu TRA.Sasa wamenipa TAX CLEARENCE FORM eti nipeleke manispaa wanipe leseni,jamani mwenye uzoefu anielimishe kwani mimi ni muumini mzuri wa kulipa kodi ingawa lengo langu kubwa ni kufanya kabiashara kangu kiuhalali mbona naona kama mambo ni mengi mno?Je,huko manispaa watahitaji nini tena?Leseni ya biashara ni shilingi ngapi?Halafu Tra wameniandikia kwenye fomu yangu RETAIL SHOP,Hicho ni nini wadau?Halafu,kwa kuwa Tin number nimepewa je,naweza kuwaona Tigo,Vodacom na Airtel ili waweze kunisajili na kuwa wakala wao ili nianze kufanya miamala ya pesa?Maana hilo ni miongoni mwa malengo yangu!